Baada ya kuaga rasmi mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Simba SC sasa wanarejea kwenye majukumu ya Ligi Kuu ya NBC, wakitarajiwa kukipiga dhidi ya KMC, maarufu kama Watoza Ushuru wa Manispaa ya Kinondoni.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1 usiku katika dimba la KMC Complex, ambapo nyasi za uwanja huo zitashuhudia pambano kali kati ya timu hizo mbili.
Kwa sasa Simba wanashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamecheza michezo saba, huku KMC wakiwa mkiani mwa msimamo baada ya kucheza michezo 14 na kuvuna alama nane pekee.
KMC ukimtoa kipa waliobaki ni kikundi cha wahuni😀😀 zile counter 3 walizopata hata kukimbia hawajakimbia wameacha mpira aisee!!! Washuke daraja tu hawafai ligi kuu