FT: Kufuzu AFCON 2023 | Niger 1-1 Taifa Stars | Uwanja wa de L'amitie, Benin

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ipo kwenye Uwanja wa Stade de L'amitie General Cotonou Nchini Benin ikipambana na Niger kwenye mchezo wa kufuzu Afcon 2023

Hadi kufikia kumalizika kwa kipindi cha kwanza Timu zote mbili zilikwenda mapumziko kwa kufungana bao moja kwa moja, Taifa Stars wakiwa wa kwanza kufunga kupitia kwa George Mpole dakika ya 18'

Niger walisawazisha kupitia kwa Daniel Sosah dakika ya 26 ya mchezo.

=============

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya Niger katika mechi ya kufuzu AFCON 2023 kwenye Uwanja wa de L’amitié Jijini Cotonou Nchini Benin, leo Juni 4, 2022.

Tanzania ilitangulia kupata bao katika dakika ya kwanza mfungaji akiwa ni George Mpole, wenyeji waliotumia uwanja wa Nchi ya jirani walisawazisha kupitia kwa Daniel Sosah dakika ya 26.

Mchezo huo ni wa Kundi F, timu nyingine katika kundi hilo ni Algeria na Uganda. Mchezo ujao wa Tanzania ni Jumatano ijayo Juni 8, 2022 dhidi ya Algeria Jijini Dar es Salaam.

 
KILA LA KHERI TAIFA STARS!!🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
83' Almanusura Taifa Stars imepigwe chuma aisee..!
 
Kwangu mimi Samata hana mchango wowote zaidi ya kuchomesha
 
Huyo Adebayor wanayemtaka Simba naona kadhibitiwa kirahisi tu na Kibwana
 
Kama huu ndio mpira watu wanaendea vibandani kila siku, na kuuongelea utadhani ni real Madrid vs Liverpool..basi hongereni.
 
87' Kennedy anaingia badala ya Feisal..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…