Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Mbiringe au Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara[emoji1241] kuendelea leo January 18, 2023 ambapo Wataalamu wa kusakata kabumbu lenye viwango vya CAF, baada ya kuweka kambi kwa siku kadhaa nchini Dubai, Wekundu wa Msimbazi, Simba SC[emoji881] wanawakabili Wabishi wa Mbeya, Mbeya City🟣 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam[emoji2522]
Simba SC kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu aliweza kuibuka na ushindi mnono wa mabao 7-1 dhidi ya Tanzania Prisons, huku Mbeya City kwenye mchezo wake wa mwisho waliambulia kisago cha mabao 6-1 dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, hivyo ni mchezo ambao unazikutanisha Timu zenye itikadi tofauti, ipo ambayo inafunga sana mabao[emoji881] na nyingine inaruhusu mno mabao🟣.
Wadau wa Soka na Mashabiki na Wanachama wa Simba SC leo hii jambo kubwa ni kuona soka la Kocha Mpya wa Simba SC Robertinho[emoji1054] akiongoza kikosi kwa mara ya kwanza kwenye michuano hii ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambaye ni muumini wa soka safi la kuvutia, huku mfumo wake pendwa muda wote ni kumpa presha mpinzani kwenye eneo lake ambapo akifanya makosa tu washambuliaji wake wayatumie.
Je City🟣 wanaweza kuhimiri presha ya muda wote wa dakika 90 bila kufanya makosa juu ya washambuliaji hatari wa Mnyama[emoji881]? Usikose Yatakayojiri.
Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku [emoji354].
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
====================
00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Benjamin Mkapa | Simba SC 0-0 Mbeya City
05' Mpira umeanza kwa kasi, huku kila timu ikijaribu kutafuta bao la mapema, City wanapoteza mpira miwili ambayo imechezwa na golikipa Manula, kama wangekuwa makini wangeweza kufunga bao..!
10' Saidooo [emoji460]Goooooooooooooaaal gooal
Ntibazonkiza anaweka kambani bao la kwanza akipokea pasi murua kutoka kwa Chama.
Mpira umeanza kuchangamka sasa, City wanatafuta kuchomoa.
13' [emoji460]Goooooooooooooaaal gooal Mbeya City wanasawazisha kupitia kwa Richardson | Simba SC 1-1 Mbeya City.
21' Awadh anashindwa kutulia eneo la lango la Simba SC, utulivu ungeweza kupata bao.
Ntibazonkiza anapiga Krosi lakini hakuna MTU wa kumalizia, ilikuwa nafasi nzuri.
25' Ni Free Kick kuelekea Simba inapigwa kulee lakini golikipa Manula anadaka bila wasiwasi.
30' Mpaka sasa mchezo ubalance kwani licha ya Simba kulifikia lango la City na City nao wanalifikia lango la Simba.
34' Anakwenda nje Chama na Bocco na nafasi zao zimechukuliwa na Sakho na Kibu.
Ulitarajia haya mabadiliko ya Chama?
Kocha anajua zaidi ngoja tuone.
43' Kanoute anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Khimbwa
Faulo inapigwa kulee lakini wanaokoa hatari ile Simba SC
45+2' Kuelekea kuwa mapumziko timu zikiwa zinashambuliana kwa zamu.
Free Kick kuelekea City anapiga Ntibazonkiza, lakini City wanazuia hatari, haya kwake Sakho.
Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC na City wanakwenda wakiwa na bao moja kwa moja.
HT: SIMBA SC 1-1 MBEYA CITY
Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa kwa kasi
Penalty kuelekea lango la City, anakwenda kupiga Ntibazonkiza
47' Ntibazonkiza [emoji460]Goooooooooooooaaal gooal..Sadio Ntibazonkiza anaweka kambani bao la pili kwa mkwaju wa Penalty
52' Madeleke wa City anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kuzozana na mwamuzi wa mchezo.
Sakho anapokea pasi murua sasa Sakho [emoji460]Goooooooooooooaaal gooal
Pape Sakho anaandika bao la tatu kwa shuti kali la masafa marefu SGR na kumuacha golikipa wa City anaruka bila mafaniko.
Mzamiru anaonyeshwa Kadi ya Njano
63' City wameruhusu Simba SC kuwasogelea kipindi hiki cha pili, huku Sakho akiwa yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha.
Kadi ya pili kwa Madeleke. Ni KADI Nyekundu baada kuchezea madhambi Sakho.
68' Onyango anaonyesha Kadi ya Njano kwa mchezo mbaya, mpira ni mkali mno
70' Sabilo akiingia kuchukua nafasi ya MTU, anapiga Krosi lakini hakuna MTU wa kumalizia ilikuwa nafasi nzuri
Kunambi anamuweka chini Sakho, Kadi ya Njano inatoka kwa upande wake, pressure ni kubwa sana wa City
78' [emoji460]Goooooooooooooaaal gooal City wanaweka bao la pili kupitia kwa Juma Shemvuni | Simba SC 3-2 City.
Almanusura City wawake chuma cha Tatu Kichwa kinapaa nje ya lango la Simba.
85' Kyombo anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali [emoji91][emoji91] kuelekea lango la City.
Sabilo anakosa nafasi nzuri, almanusura afunge bao, mashambulizi ni makali wa pande zote mbili.
90+4' Kyombo anatoka na ameingia Nyoni upande wa Simba SC.
Wakati wowote mpira utamalizika refa anaagalia saa yake.. Naaaaaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Mbeya City.
FT: SIMBA SC 3-2 MBEYA CITY
...... Ghazwat...