FT: Pre-season | Simba SC 2-0 Al Akhaood Club International Friendly Match | Misri

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Wekundu wa Msimbazi Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, katika kuendelea kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa na Simba Day, leo Agosti 1, 2022 amejitupa uwanjani kucheza na Al Akhaood Club kutoka Saudia Arabia, kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki, ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila, mchezo uliopigwa Jijini Ismailia nchini Misri, mabao yakifungwa na Gadiel Michael na Augustine Okrah.

Huu ni mchezo wa mwisho wa kirafiki wa kimataifa kwa Simba SC kuchezwa wakiwa Misri, ambapo Agosti 4, 2022 kikosi kinatarajia kurejea Jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya Simba Day.



 
Aliburuza na magoti bila kujali visiki vya uwanja

Kambole kwa kufunga goli moja tayari mwenzetu kaishafunga mahesabu

Kila mwaka lazima atupie goli moja kwa hiyo huu mwaka hana deni tena
Hata alipomtungua Manula msimu ulipita aliburuza magoti kama ulitazama vizuri

Huyu jamaa mjinga sanaa
 
Uzi umetulia vibaya mnooo.. Hii ndio jezi sasa
 
KIPIMO CHENU NI WALE WAARABU WENGINE, HAO WA KAWAIDA TU...
 
Yanga wanacheza mechi hawatoi hata line up na wachambuzi wa mchongo wamekaa kimya tu angefanya simba vile.
 
Yanga wanacheza mechi hawatoi hata line up na wachambuzi wa mchongo wamekaa kimya tu angefanya simba vile.
Line Up? Hiyo ratiba kuijua mbinde, unashtukia tu baada ya game Yanga amla mtu 9 yaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…