FT: Sudan Premier League | Al Hilal Omdurman 4-0 Wad Nubawi SC | Al Hilal Stadium 12/10/2022

FT: Sudan Premier League | Al Hilal Omdurman 4-0 Wad Nubawi SC | Al Hilal Stadium 12/10/2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Klabu ya Al Hilal Omdurman ya nchini Sudan [emoji1232] imecheza mchezo wa Ligi Kuu Sudanese Premier League (SPL) kwenye uwanja wake wa nyumbani Al Hilal Stadium, dhidi ya Wad Nubawi SC, na kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao manne kwa bila 4-0.

Al Hilal Omdurman wanatarajiwa kucheza na Yanga Africans, kwenye mchezo wa marudiano wa michuano ya Mabingwa Afrika (CAFCL) Jumapili ya Oktoba 16, 2022 kwenye Dimba la Al Hilal Stadium.

Je, Simba SC na Yanga SC na Azam FC wanaweza kucheza mchezo wa Ligi Kuu siku tatu kabla ya kucheza michuano ya CAF?

NB: Ligi ya Tanzania [emoji1241] ina mapumziko sana yasiyokuwa ya kawaida.
20221012_234624.jpg
 
Wanaweza Sana tu , sema tifua tifua ndio wanafanya ligi inasimama , kwa kisingizio kua simbwa na yambwa wanajiandaa na club bingwa Africa

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
Ujinga tuu unatusumbua. Yule bwana kasongo mwanzo wa ligi kujitapa kwingi kuwa tumeshapanga ratiba vizuri hamna viporo lakini wapi.
 
Ukisikia Bongo nyoso ndio hii sasa , maneno mengi , vitendo mswaki

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
Na tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu tuu. Leo hii tunafungwa na south sudan kweli....watu wamepigana vita wamemaliza na wanakuja kutufunga wanaenda zao afcon.

Kule india nako balaaa...tumeenda na under 30 tumefungwa na u17 wa ukweli. Hatujui tunalolifanya.
 
Klabu ya Al Hilal Omdurman ya nchini Sudan [emoji1232] imecheza mchezo wa Ligi Kuu Sudanese Premier League (SPL) kwenye uwanja wake wa nyumbani Al Hilal Stadium, dhidi ya Wad Nubawi SC, na kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao manne kwa bila 4-0...
Viongozi wa soka bongo vichwani sifuri,wao wanaongozwa na vilabu badala ya wao kuviongoza! Na viongozi wa vilabu bongo vichwani Ziro wanaongozwa na vimuhemuhe.

Hawajifunzi kutokana na makosa ,Simba ilitolewa na Orlando Pirates mwaka juzi kwa kukosa match fitness baada ya kukaa wiki mbili bila kucheza Matokeo yake ikapigwa 4-0 soweto baada ya kuwa wameishuhudia Orlando ikicheza mechi ya ligi katikati ya wiki wakiwa hukohuko south Africa,.

Mwaka Jana pia Jwaneng Galaxy wamekuja kumtoa Simba Taifa wakiwa wametoka kucheza mchezo wa ligi yao katikati ya wiki, huku Simba ikiusubiria mchezo wao na Bado Simba ikapigwa 3-1 Taifa na kutolewa CCL ! Viongozi wa soka bongo ni vilaza kupindukia hawana mipango wao ni mihemko tu .

Majuzi nilimsikia kocha wa Yanga,Nabi Akilalamikia ratiba baada ya mechi ya Kwanza na Zalan baada ya kuwa wametoka kucheza na Azam katikati ya wiki na kutakiwa kucheza mchezo wa ligi kabla ya mechi ya marudiano na Zalan, naona wakamsikiliza na kupangua ratiba.

Vilaza sana yaani hawana mipango,dira Wala naona ni kupelekwa Kama mang'ombe tu
 
Na tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu tuu. Leo hii tunafungwa na south sudan kweli....watu wamepigana vita wamemaliza na wanakuja kutufunga wanaenda zao afcon.

Kule india nako balaaa...tumeenda na under 30 tumefungwa na u17 wa ukweli. Hatujui tunalolifanya.
Sonamalia na south sudan teams zao za vijana ni watoto waliozaliwa ukimbizini ulayaa
 
Ujinga tuu unatusumbua. Yule bwana kasongo mwanzo wa ligi kujitapa kwingi kuwa tumeshapanga ratiba vizuri hamna viporo lakini wapi.
Kila wakijaribu kupanga kusiwe na viporo wanachemka, lakini wakati wakipanga ratiba yao wanasema tumezingatia Kalenda ya FIFA kwa timu ya Taifa na mechi za Kimataifa kwa vilabu.
 
Back
Top Bottom