FT: Tanzania Prisons SC 0-1 Yanga SC | Ligi Kuu ya NBC | Kwa Yanga Hii Mtasubiri Sana

Holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
8,723
Reaction score
19,715
Yanga kama kawaida imeendeleza makali na kubaki kileleni katika Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Tanzania Prisons ya Mbeya Goli 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, leo Machi 12, 2026, hivyo kufikisha pointi 35 katika mechi 13.


============

Wakali, vinara, mabingwa wa kihistoria na mabingwa watetezi wa NBC PL, Young Africans SC watakuwa ugenini katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma wakicheza na wajelajela kutoka Jijini Mbeya, Tanzania Prisons SC saa 2:00 usiku.

​
Ambatana nami sako kwa bako kukuletea updates za mchezo huu muhimu na wa kihistoria mjini Tabora.

Ujumbe: Yanga Bingwa.


FT: Yanga ikiwa ugenini imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kwa ushindi huo Yanga inaendelea kujikita kileleni ikifikisha alama 35 huku Tanzania Prisons ikisaliwa na alama 13
 
Kila la kheri kwetu Wananchi japo taarifa zako zinakinzana na za kwenye Kurasa za Kijamii za timu yetu.

Hebu fuatilia kisha U-edit basi Mkuu.

#DaimaMbeleNyumaMwiko.
nirekebishe tu mkuu si wote tulio na uwezo wa kuifikia mitandao hiyo.
 
Sijakuelewa hata Mkuu.
mimi natumia simu ndogo yenye file la opera min, ndilo natumia kuingia JF, so fb,twiter sijui wapi huko huwa siwezi kuingia huko kutokana na changamoto ya simu mkuu! So kama nimekosea mahala nirekebishwe
 
mimi natumia simu ndogo yenye file la opera min, ndilo natumia kuingia JF, so fb,twiter sijui wapi huko huwa siwezi kuingia huko kutokana na changamoto ya simu mkuu! So kama nimekosea mahala nirekebishwe
Ooh. Sawa.

Japo kikawaida wenye uwezo wa kuedit uzi ka hivyo ni wewe mwenyewe mleta uzi na Mods.

Hivyo usijali Mkuu, Mods wakiona wataliweka hili sawa.
 
Ooh. Sawa.

Japo kikawaida wenye uwezo wa kuedit uzi ka hivyo ni wewe mwenyewe mleta uzi na Mods.

Hivyo usijali Mkuu, Mods wakiona wataliweka hili sawa.
hivi ni Dodoma ama tabora? kama ni Dodoma basi itakuwa ni usiku.
 
Hii mechi saa 10 au saa 2 usiku!?
 
GEMU::-
Saa Mbili 2:00 Usiku....
Jamhuri Idodomya...
Tz Prisons Vs Young Africans..
​
 
HT : 45'
Nyie prison mjue tu kuwa wapo watu wamezichafua Meza kwa Monde muda huu....! 'Wanapiga vyombo'... huku wakifatilia kwa karibu kipute..


Kazeni hivyo hivyo..., wasaidieni wajasiriamali hawa wenzenu wauzaji wa Monde ili Meza ziendelee kuchafuka...!

Yaani 'Monde' ikiambatana na Yanga kupoteza au kupata sare huwa inanoga vibaya.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…