OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Bao la Vivian Corazone limetosha kuipa Simba pointi tatu muhimu dhidi ya mtani wake ambaye kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa mnyonge.
Katika Ligi Kuu ya Wanawake Yanga haijawahi kuifunga Simba ndani ya misimu mitano, mara ya mwisho ikiwa ni 2018 kwa ushindi wa bao 1-0.
Tangu 2018 mchezo wa leo baina ya wababe hao ni wa 13 lakini Yanga imeambulia ushindi mara moja tu huku ikifungwa mara 9 na kutoa sare mara tatu.