Fuata mwongozo huu kabla hujanunua TV. Utanishukuru baadae

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,914
Reaction score
168,320
Copied from facebook

USINUNUE TV KWA KUKURUPUKA FUATA MWONGOZO HUU
Kwenye maduka ya vifaa vya kielektroniki, kuna mtego mkubwa sana unaowatasa watu wengi wanaotafuta TV za bei nafuu. Mteja anaingia dukani na bajeti ndogo, anaona TV ya inchi 43 au 50 ikiwa imeandikwa "4K Smart Android" kwa bei ya kuokota. Anafurahi na kuona amepata mchongo wa maisha, lakini miezi mitatu baadaye TV inaanza kugoma kuwaka, mfumo unagandaganda (freezing), na picha inafifia kama picha ya simu ya zamani!

Ili usije ukaponza jasho lako, huu hapa ni mwongozo kamili utakachokusaidia kuchagua TV sahihi kulingana na chumba chako, ubora wa picha, vijenzi vya ndani, na aina ya brand unayotakiwa kuinunua:

Ukubwa wa Skrini kulingana na Chumba Chako

Watu wengi wanadhani TV kubwa zaidi ndiyo bora zaidi, lakini ukweli ni kwamba ukubwa wa skrini unatakiwa uendane na umbali wa mahali unapokaa (Viewing Distance):
Chumba Kidogo (Mita 3x3):
Saizi Sahihi ni Inchi 32 hadi Inchi 43.
Umbali kati ya sofa na TV kwenye chumba hiki ni mita 1.5 hadi 2. Wazo la kuweka TV ya inchi 55 au 65 hapa litakuumiza macho na kukupa maumivu ya kichwa kwa sababu uko karibu mno na skrini.

Sebule ya Kati (10m² hadi 18m²):
Saizi Sahihi: Inchi 43 hadi Inchi 55.
Hii ndiyo saizi ya kawaida kwa nyumba nyingi. Unakuwa na umbali wa mita 2 hadi 2.5 kutoka kwenye skrini, unaokupa fursa ya kuona picha yote vizuri bila kuchosha macho.

Sebule Kubwa (20m² na kuendelea):
Saizi Sahihi: Inchi 65, 75 hadi 85+
Kama una sebule kubwa yenye umbali wa mita 3+ kutoka ukutani hadi kwenye sofa, TV ndogo ya inchi 43 itaonekana kama monitor ya kompyuta. Hapa ndipo skrini kubwa zinapoleta muonekano halisi wa jumba la cinema (Home Theater Experience).

Ubora wa Picha (Resolution)
Resolution ni idadi ya nukta za picha (pixels) zilizopo kwenye skrini. Ukubwa wa skrini ndio unaoamua unahitaji resolution gani:

HD Ready (720p): Inatosha kabisa kwenye TV za Inchi 32. Kwenye skrini ndogo, jicho la mwanadamu haliwezi kutofautisha kati ya 720p na 1080p.
Full HD (1080p): Hii ndiyo kiwango cha chini kinachotakiwa kwa TV za Inchi 43. Picha inakuwa safi na yenye mikato ya wazi.
4K Ultra HD (2160p): Ni LAZIMA kwa TV yoyote ya Inchi 50 na kuendelea. Skrini ikiwa kubwa bila kuwa na 4K, picha itaonekana imevutika, ina vumbi, na haina makali (pixelated).

Vifaa vya ndani alya TV
Hapa ndipo wauzaji wanapowapiga wateja wengi. Mfumo wa TV kwa nje unaweza kuonekana mzuri, lakini ndani ukawa na vipuri vya hovyo:

RAM na Memory (RAM & Internal Storage): Kama unanunua Android au Google TV, usikubali TV yenye RAM chini ya 1.5GB au 2GB. TV zenye RAM ya 512MB au 1GB zitaanza kuganda (freeze), kurusha Apps nje, na kuchukua dakika kibao kufungua mfumo baada ya miezi michache tu.

Processor (Chipset ya Picha): TV nzuri zinasindikiza picha kwa kutumia Processors za kisasa za AI. Zina uwezo wa kuchukua video ya ubora wa chini na kuiongezea ubora (upscaling) ili ionekane safi. TV za bei rahisi hazina mfumo huu, ndio maana mpira ukirushwa unaona unawacha kivuli nyuma!

Makundi 3 ya Brand za TV Sokoni (Uchaguzi wako wa Duka)

Sokoni kuna makundi matatu makuu ya brand za TV, na hapa ndipo unapotakiwa kufanya maamuzi ya akili:

1-LG, Sony, Samsung
Ukweli Wake: Hawa ndio wafalme wa teknolojia ya skrini duniani (OLED, QLED, na Processors za hatari). Zina picha safi sana, zinadumu miaka na miaka, na hazigandi.
Ushauri: Kama mfuko wako una uwezo, nunua hapa bila kusita!

2 Budget Kings (Hisense, TCL, Haier)
Ukweli Wake: Hili ndilo kundi bora zaidi kwa Mtanzania anayetaka TV nzuri kwa bajeti ya kati. Zina ubora mzuri wa picha, mifumo imara (Google TV / Android / VIDAA), na hazina matatizo ya mara kwa mara.
Ushauri: Kama huna fedha za kutosha kununua Tier 1, kimbilia Tier 2. Hapa utapata thamani halisi ya fedha yako!

3 Alitop, Sundar, Amochi, Star X, n.k.
Ukweli Wake: Hizi ndizo TV za "kopo" au mtego wa mtaani. Zinaandikwa sifa za uongo kwa nje (kama 4K feki), zina RAM ndogo ya 512MB, bodi zake ni nyepesi kuungua, na picha zake zimefifia.

Ushauri: Hili ndilo kundi BABA LA MATATIZO. Ziukimbie brand hizi kama ukoma! Ni bora ununue TV ndogo ya Tier 2 kuliko kununua inchi kubwa ya Tier 3.

🤔 Je, chumba au sebule yako ina ukubwa gani, na kwa sasa unatumia TV ya kundi gani kati ya hayo matatu? Dondosha maoni yako hapa chini tuone kama ulichagua saizi na brand sahihi!
 
Namna ya kuiwezesha tv isiyo smart kuweza kuacess mtandao ua kuifanya iwe smart?
 
HISENSE SIYO TV NI UCHAFU
 
Sisi tulio na SOLARMAX ambazo sio smart 24" tusemeje?
 
elezea zaidi mkuu hapa : bei, kuset au install
 
Eeh hapo kwenye nchi 15 ni jambo la kufikiria sana, mimi naona 32" inatosha chumba cha kawaida. Solarmax zenu hizo ni noma kama hazina smart, ila ikiwa na HDMI port unaweza connect Android box
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…