Fuatana na Xi Jinping kusherehekea sikukuu ya Duanwu

Fuatana na Xi Jinping kusherehekea sikukuu ya Duanwu

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1593072908477.png
TIM图片20200625161258.jpg

Wachina wanasherehekea sikukuu ya Duanwu kwa njia mbalimbali za kijadi ikiwemo kuweka vifuko vidogo vilivyojazwa manukato na dawa za mitishamba kwenye nguo zao, kula Zongzi ambacho ni chakula cha mchele unaonata uliofungwa kwa majani ya matete, na kufanya mashindano ya mbio za mashua ya dragon.

Kuweka vifuko vidogo vilivyojazwa manukato kwenye nguo ni mila yenye historia ya zaidi ya miaka elfu 1, watu wanafanya hivyo ili kutakiana salama na kuepusha magonjwa. Mzee Wang Xiuying mwenye umri wa zaidi ya miaka 80 ni mrithi wa utamaduni usio wa vitu kwa ustadi wake wa kutengeneza vifuko hivyo.

Septemba mwaka 2017, rais Xi Jinping wa China alikagua kijiji cha Mazhuang. Rais Xi alisifu sana vifuko vidogo vilivyojazwa manukato vilivyotengenezwa na wanakijiji, na alinunua kifuko kilichotengenezwa na bibi Wang Xiuying.
 
Back
Top Bottom