Nimefuatilia comments zenu wote, kila mtu jibu analikaribia jibu ngoja tuwekane sawa hapa kwanza jua kwamba injini ikisha washwa mafuta ni lazima yatumike hata kama ni kwa kiasi kidogo lakini ni lazima ya tumike
Kuhusu kwenye D na N,,hapo kwenye ulaji ni lazima utofautiane ijapokuwa ni kwa kiwango kidogo sana,gari ikiwa kwenye N maana yake ni injini tu inayozunguka kwahiyo gari itakuwa na mzigo wa kuzungusha injini tu
- ila gari ikiwa kwenye D au Drive maana yake injine imeshakuwa connected na difu ya gari maaana yake hapa sasa gari itakuwa na kazi mbili za kufanya yani kuzungusha injini pamoja na matairi yake kwahyo ni lazima compression kwenye injini iongezeke ili kuzungusha difu ndo results ya matairi kuzunguka kwa maana hiyo ni lazima ulaji wa mafuta kwenye D uwetofauti na wa N
Huku ninapoishi kuna kampuni flani ya usafirishaji wa mizigo na baadhi ya madereva ni rafiki zangu katika stori stori huwa wanasema kabisa ukitembelea mara nyingi N safarini lazima upate mafuta mengi yanayobaki na hivyo jamaa huwa wanayatoa na kuuza na huwa wanapata hadi elf 70 hadi 50 kwenye mafuta tu per root
Ingawa kitalaamu,watalaam wameonya usipende kutembelea N mara kwa mara,gearbox inaweza pata itirafu.asanteni