MWananyati
Senior Member
- Feb 3, 2011
- 160
- 53
Kwa kweli kama Hayati mwalimu alitabiri kwa uhakika kabisa kuwa serikali ikishikwa na wafanya biashara utoaji wa maamuzi utakua mgumu. Na akataka siasa itenganishwe na biashara. He was right.
Wafanya biashara wa mafuta wameamua kwa ujeuri wao kuwatesa Watanzania. Bei kushushwa tu kidogo, bila hata kuathiri faida yao, wameona jambo hilo si sawa, na kuamua kugoma. Haijawai tokea wafanyabiashara hawa, kupinga pindi serikali inapoongeza bei ya mafuta. Tunateseka.
Serikali tafadhali mfanye maamuzi magumu. Na kwa namna tatizo lilivyojitokeza, nategemea mtakua mmejiandaa kukabiliana na hali hii. SIFIKIRI, NA HAIINGII AKILINI KAMA KWELI SERIKALI INAYOONGOZA WATU ZAIDI YA MILIONI 40 ITAWAPIGIA MAGOTI WAFANYABIASHARA HAWA AMBAO WAMEUKOSA UTU, NA KUONESHA DHARAU YA WAZI KWA SERIKALI.
Ni wakati wa kurekebisha sheria nyingi ili ziwabane wafanyabiashara. na hili litawezekana iwapo wafanyabiashara watakaa mbali na siasa. Wafanyabiashara wanatikisa nchi kwa kutumia migongo ya wanasiasa. Tumechoka
Rais wetu, tafadhali huu ndio wakati wako. Fanya uamuzi sahihi kuwasaidia Watanzania, Sipendi na sitaki kuona hasira ya Watanzania ikiwaka juu yako.
Wataalam, wanasheria saidieni tupate ufumbuzi wa haraka wa tatizo hili
Asante