Fuel gauge kugonga juu Toyota Corolla

Fuel gauge kugonga juu Toyota Corolla

LIFE HELP

Senior Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
149
Reaction score
71
FUEL GAUGE KUGANDA JUU TOYOTA COROLLA

Naomba msaada gari almost mpya 6000 km tu toka Japan nimeipokea , ikiwa na mafuta kidogo sana taa ya empty inawaka lakini gauge iko full tank,

Nikashauriwa labda sababu ya kukaa muda mrefu itakuwa ime stuck tu , weka mafuta full tank then kadiri unavyotumia boya la gauge linaweza kuachia kwa kugongwa na mafuta,

nikafanya hivyo full tank 43 ltr na taa ikazima, lakini hadi leo ni wiki sasa na nina 240 km
naamini mafuta sasa yanacheza vya kutosha bado gauge iko pale pale inasogea kidogo sana kama 3 mm kwenda juu

Wapi kuna mafundi wazuri DAR wenye workshop ya kisasa angalau yawezekana sio boya labda ni WIRING SYSTEM ,

Naombeni ushauri
 
Back
Top Bottom