Fukuza fukuza ya walimu

Msingida

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
10,239
Reaction score
11,731
Hili la Waziri Kassim Majaliwa na Mulugo kuwafukuza walimu wakuu wa Ilboru na namkukwe chunya mbona linatia shaka taratibu za utumishi?Mamlaka zinazo husika mbona zimefunga midomo?Siwatetei wakosaji lakini kanuni na taratibu zifuatwe ilikuweza kuwatendea haki.Bado tunawahitaji walimu ndo maana wizara ya Elimu imetoa mwaliko kwa walimu kutoka nchi za jirani kuja kuwafundisha watoto wetu.Japo nchi hizo zina walimu feki ukilinganisha na hapa kwetu,lakini bado hatuwajali na kuwatendea haki.Tunataka kuleta kasumba mpya ya mawaziri wanaofukuza wafanyakazi majukwaani ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.Mamlaka zinazo husika kutetea haki ya wafanyakazi waingilie kati maswala haya na kuwaburuza mahakamani mawaziri ili iwe fundisho kwa mawaziri hao ambao wanasubiria kuwafukuza watumishi majukwaani.
 
Je huyo Mwl. Mkuu amefukuzwa au amesimamishwa?
 

mkuu je umechunguza alichokifanya ndio akasimamishwa kazi?na je kama amefanya jambo lisilohitajika kisheria, apotezewe kwa sababu walimu ni wachache?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…