FULL REPORT: Black Sailor 0 Simba SC 4

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Jeshi la maangamizi lilokua vitani jana usiku katika uwanja wa Amaani.

View attachment 272572

Kikosi bora kabisa kwa sasa Zanzibar, Black Sailor ambao wamepanda ligi kuu msimu ujao kwa kuvunja rekodi ya kua na point nyingi.. Naimani msimu ujao ni mabingwa.

View attachment 272573

Jopo la ufundi, likihakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa katika mechi dhidi ya Black Sailor.

View attachment 272574

Mchezaji wa Simba SC akiwa kazungukwa na kijiji

View attachment 272575

Mshambuliaji tegemeo kabisa wa Black Sailor, akijaribu kuupita Great Walll of China, kilichomkuta siwezi hata kuhadithia.

View attachment 272576

Kiungo Bora kabisa kwa sasa, Abdi Banda akinyanyua mashabiki waliofurika katika uwanja wa Amaani, kwa goli safi la kichwa (goli la kideoni)

View attachment 272578

Hamis Kiiza Aguerro (mwenye jezi 5) na wachezaji wenzake wakimpongeza Banda kwa kufunga goli la kwanza.. Kiiza ndo alipiga krosi, Banda akatupia.

View attachment 272584

Huyu beki wa Black Sailor, baada ya kuzidiwa kila kitu, na Kiiza.. Akaamua kucheza rugby.

View attachment 272588

Huyu nae anajaribu kumzuia Mgosi, sijui hafahamu kua Mvinyo wa kale ndo dili?!

View attachment 272592

Ibrahimu Ajibu "Hat-trick Master" akifunga goli la pili.

View attachment 272593

Ilikua ni vita kweli kweli, ukikamata mpira tu.. Unakabwa na wawili wawili.

View attachment 272594



MWISHO WA SIKU:

Mnyama mkali sana mwituni, asiyekua na masihara anapokutana na kitoweo mwituni alishinda goli 4-0. Magoli ya simba yalifungwa na Banda, Ajibu, Maguli na Isihaka.
Taarifa nilizozipata toka Katika chanzo changu cha uhakika kilichokua uwanjani, ni kua jana Simba SC imeonesha soka la uhakika ambalo halijaonekana katika visiwa hiyo kwa mda mrefu sana.. Lilikua ni la kasi kubwa sana (zaidi ya speed of light) likijaaa pasi fupi fupi zenye macho, huku kiiza, banda, mwalyanzi, mkude, ajibu wakifanya waliofika uwanjani kua wanasimama kila Mara kushangilia vitu adimu walivyokua wakionesha.
Shukrani kubwa ziende kwa golikipa wa Black Sailor pamoja na beki wake kwa kuzuia kufungwa goli si chini ya kumi.

HALI ILIVYO SASA:

WAO.. View attachment 272596

SISI… View attachment 272597

NOTE: Leo tena Simba SC atakua uwanjani kupambana na Polisi wa Zenji.

Credit: Zanzinews
 
asante mkuu kwa kutujuza Simba chama kubwa
 
Nashukuru mkuu kwa taarifa nzuri.

Tulikuwa wote jana pale uwanjani na nilikuwa naona vijana wetu wa msimbazi wakitandaza soka la kimataifa zaidi ila nikurekebishe tu mkuu pale jana jonasi mkude hakwepo ni mgonjwa ila leo tunatarajia kumuona kionga bora kabisq ukanda huu wa afrika mashariki na kati si mungne ni Haruna moshi boban atakwepo leo tutakuwa pamoja mwanzo mwisho wa mtanange.

SIMBA NGUVU MOJA
 
Baadhi tu ya picha za jana
 

Attachments

  • 1438353099367.jpg
    45.9 KB · Views: 190
  • 1438353180109.jpg
    48.8 KB · Views: 177

Mkuu hata mi nimesikia kua Mkude, ameumia enka.. Ila unataka kuniambia Boban, katua rasmi Simba Sc?
 
Mkuu labda itakua ni mtandao tu.. Ila zinafunguka.

Wimbi la ushindi la simba sc linaendelea bado na leo tumetoa dozi ya goli mbili bila majibu kwa polisi ya zanzibar magoli yakifungwa na Mussa mgosi kipindi cha kwanza na Elias manguli kipindi cha pili na mpaka dk90 refa anamaliza mtanange simba 2 polisi 0 pia tumeshuhudia kiungo machachari kabisa mwinyi kazimoto akiwa na klabu yake ya zamani ya simba tayari kujiandaa na mazoezi natumaini jumatatu ktk mechi ya kirafiki atakwepo uwanjani
 

Mkuu asante sana kwa taarifa.. Simba sasa imenoga.
 
Hii timu imeshakuwa ya kucheza vimechi na vitimu vidogodogo ubingwa na nafasi ya pili wataisikia redioni na kusoma magazetini
 
hii samba imekua mdeadly hivi...
haaa haaa kaazi kweli kweli
 
Mkuu hizo ni tetesi.. Tuwe wavumilivu, na tuombe isitokee.

Jana simba ilicheza mechi yake ya tano ya kirafiki na kuifanya vizuri tena kwa mara ya tano ushindi mfululizo kwa kushinda goli 3 dhidi ya 2 za KMKM ikicheza mpira mzuri zaidi na wa kisasa zaidi uwanjani huku mashabiki wakishangilia sana
 
Jana simba ilicheza mechi yake ya tano ya kirafiki na kuifanya vizuri tena kwa mara ya tano ushindi mfululizo kwa kushinda goli 3 dhidi ya 2 za KMKM ikicheza mpira mzuri zaidi na wa kisasa zaidi uwanjani huku mashabiki wakishangilia sana

Mkuu hii Simba ya sasa, ni ya ULAYA.. Ushindi mwanzo mwisho.. Kitoweo chetu kinachofuata ni AFC Leopards, 08/08/2015.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…