Full Text: Alichosema CEO wa Simba SC Crescentous Magori

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
ALIYOSEMA AFISA MTENDAJI MKUU CRESCENTOUS MAGORI KWENYE MKUTANO NA WANAHABARI.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jana tarehe 12 June kilifanyika kikao cha Bodi ya Simba Sports Club Company Limited. Kikao hiki kilifikia maazimio mbali mbali juu ya maendeleo ya Klabu yetu.

1.0 Taarifa juu ya maendeleo ya mabadiliko ya muundo wa Klabu kuwa kampuni ( Transformation)

Itakumbukwa kuwa Klabu ilijipa muda wa mpito ( transition) wa kukamilisha ubadilishaji wa muundo wa mabadiliko ya Klabu kuwa Kampuni. Bodi imeridhika na hatua iliyofikiwa ya ukamilishaji wa muundo wa Kampuni na imeongeza nguvu kazi ya ukamilishaji wa muundo wa Kampuni. Bodi imewateua Aziz Kefile, Mulamu Ng’ambi, Barbara Gonzalez, na Wanasheria wa Kampuni ya Simba Evodius Mtawala na Michael Mhina kukamilisha kwa haraka hatua ndogo iliyobaki. Ni matarajio ya Bodi kuwa ndani ya miezi miwili kila kitu kitakuwa kimekamilika.

2.0 Bunju Project

Bodi imepokea taarifa ya maendeleo ya sehemu ya mazoezi ya Klabu ya Simba iliyoko Bunju ( Training centre). Baada ya mvua kumalizika matengenezo ya kuandaa uwanja kwa ajili ya kuweka nyasi bandia yataendela, sambamba na ujenzi wa vyumba vya kubadilishia nguo ( changing rooms), na uwanja wa nyasi za kawaida.

Sambamba na hilo Bodi imemteua aliyekuwa Meneja wa zamani wa Simba Richard ......kuwa Msimamizi wa Mradi wa maendeleo wa Bunju.

3.0 Kandarasi ya jezi za msimu wa 2019/20

Bodi imepitisha mapendekezo ya kamati ndogo ya Bodi iliyoundwa kutafuta Mzabuni wa jezi za Simba kwa msimu ujao wa Ligi. Baada ya ushindani wa Makampuni matatu Novum Pharm ( Starbalm), Umbro na UHL ( Romario), Kampuni ya UHL Romario imeshinda Zabuni hiyo. Mkataba utasainiwa hivi karibuni na baadaye uzinduzi wa jezi mpya ya msimu ujao utafanyika.

4.0 Maandalizi ya pre season training na Simba week

Wakati wowote taarifa ya Timu itaenda wapi kwa ajili ya pre season training mtajulishwa. Bodi imeunda Kamati ndogo kufanya maamuzi kwa niaba yake juu ya pre season training.

Simba week ya Mwaka huu 2019 itaanza tarehe 1/8/2019 kwa kushirikisha WanaSimba na Watanzania wote nchi nzima. Mchezo wa kuhitimisha Simba week ambayo ndiyo itakuwa kilele cha Simba week maarufu kama Simba Day itakuwa tarehe 8/8/2019. Timu ambayo imealikwa mtajulishwa ijumaa hii. Bodi pia imeteua kamati ndogo ya Simba Week kufanya kazi kwa niaba yake.

5.0 Usajili kwa msimu ujao 2019/20

Bodi imepokea na kupitisha maendeleo ya hatua ya usajili ilipofikia. Na imebariiki kamati ndogo ya usajili iliyoteuliwa na Mwenyeki wa Bodi.

Usajili kwa Wachezaji wa ndani umekamilika kwa asilimia 90. Sasa mashambulizi yameanza kwa Wachezaji wa nje ya nchi. Taarifa za Wachezaji waliosajiliwa zitakuwa zinatolewa kila leo kupitia kurasa za Mitandao ya Simba kila leo.

6.0 Kadi za Wanachama ( Members card) na Wapenzi (Fans card)

Bodi imepitisha mpango wa uzinduzi wa kadi mpya za Wanachama na Wapenzi wa Simba. Uzinduzi huu unatarajiwa kufanyika ndani ya siku 10 kuanzia leo.

Nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Kampuni

7.0 Itakumbukwa kuwa iliyokuwa Bodi ya muda ya Klabu ya Simba ( Interim Board) ilimteua Ndugu Crescentius Magori kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Klabu kwa kipindi cha Miezi 6.

Bodi imeridhia matakwa ya Ndugu Magori kutoendelea na kazi hiyo na imemuomba kwa kipindi cha miezi miwili( siku 60) aendelee ili Bodi pamoja na yeye mwenyewe wasimamie upatikanaji wa Mtendaji Mkuu mpya pamoja na Waajiriwa wengine.

Hivyo nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simba pamoja na Wakurugenzi zitatangazwa kwa Watanzania na wasio Watanzania hivi karibuni. Tunatoa rai kwa watu wenye uwezo na vigezo vya kufanya na Kampuni ya Simba kutosita kuleta maombi punde kazi zitakapotangazwa.
 
Kila la heri watani zetu mambo haya ya kuendesha timu kisasa yatatusaidia sana siku zijazo, Simba na Yanga ni timu bora kabisa hapa Africa mashariki mkazo tuufanye sasa katika ngazi ya vilabu tufikie kwa wenzetu kama Tp Mazembe, Asec, Ahly, Esperance , Mamelodi na wengine, ndugu yetu Azam ajifunze hata kwa Zesco why yeye
 
VIP madai ya freedom fighter mzee kilomoni yamezungumziwa?
 
Mimi sio jamaa we mjinga, mpumbavu kweli we usitake Nafikiri Kama unavyifikiri wewe
Kamdharau mama yako unanidharau mimi unamchango gani kwangu

Acha kuzoea watu kijinga
We jamaa, nimekudharau sana hivi unadhani serikali ni wapuuzi kubadilisha uuzwaji wa hisa za Simba kwa Mo kutoka 51 hadi 49?
Fikiri mara mbili mbili kabla ya kuandika pumba
 
Mimi sio jamaa we mjinga, mpumbavu kweli we usitake Nafikiri Kama unavyifikiri wewe
Kamdharau mama yako unanidharau mimi unamchango gani kwangu

Acha kuzoea watu kijinga
We fala mkata mauno Sinza meeda bar unataka battle ya matusi?
Unataka nikukaze bi Happy?

Funguka nikuonyeshe undava wangu mnuka shombo ya K UMA wewe
 
We jamaa, nimekudharau sana hivi unadhani serikali ni wapuuzi kubadilisha uuzwaji wa hisa za Simba kwa Mo kutoka 51 hadi 49?
Fikiri mara mbili mbili kabla ya kuandika pumba
Huyo jamaa ni mseng.e analeta ushabiki wa Simba na Yanga kwenye mambo ya msingi
 
Huyo jamaa ni mseng.e analeta ushabiki wa Simba na Yanga kwenye mambo ya msingi
Analeta ushamba kwenye vitu vya kijanja anafikiri watu wamekurupuka.
Kubabake majitu kama haya huwa yananikoma nalifata kila sehemu litakapokomenti nalichafulia hali ya hewa.

Mpira halijui pumbavu
 
We ni mjinga watoto wa juzi akili zimejaa matope
Jitutumue mitandaoni lakini huna tofauti na kijana mpumbavu
We fala mkata mauno Sinza meeda bar unataka battle ya matusi?
Unataka nikukaze bi Happy?

Funguka nikuonyeshe undava wangu mnuka shombo ya K UMA wewe
 
Huyu Crenscentious Magori si ndio yule aliepiga hela za NSSF yeye pamoja na Dr.Ramadhani Kitwana Dau
crensetious magori huyo huyo alipiga kweli huko unapopasema ila huyo mtu ni simba lia lia hela ake nyingi kaitumia simba hapohapo hao ndo wanzilishi wa kundi la friends of simba lililokua linasaidia simba kipindi chote cha matatizo miaka nyuma..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…