FULL TEXT: Maelezo ya Ushahidi wa Luhaga Mpina kwa Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson juu ya Waziri Hussein Bashe kusema Uongo Bungeni kuhusu Sukari

JPM kabaki na Mpina tu anayetembea kwa hatua zake, wengine wote njaa ni kali washauza kambi.

Mpina anafaa 100% kuchukua form ya urais kwa ticketi ya CCM 2025.

Naunga mkono hoja.
 
Hivi huyu Hussein Mohamed Bashe (MB) kimemtokea nini hasa?

Kabla ya kuingia serikalini, akiwa Mbunge tu wa Nzega, alikuwa miongoni mwa wabunge bora na machachari wa CCM wenye uwezo wa kujenga hoja zenye mantiki.

Bila shaka ndicho kilichomfanya Hayati Rais John P. Magufuli amwingize serikalini kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na sasa ni full minister.

Mbona amejiingiza kwenye kashfa mbaya hivi? Na ukimtazama na kumsikiliza anavyoongea hata sasa unaweza kufikiri ni mtu wa maana mwenye maadili lakini kumbe ni shida kiasi hivi?

Au wasaidizi wake kutoka ktk taasisi zilizo chini ya wizara yake za zenye mandate ya kusimamia sekta ya Sukari nchini hususani Bodi ya Sukari (SBT) wame - blackmail? Hotuba na taarifa zake zinakinzana na uhalisia kama tu ushahidi uliowasilishwa na Luhaga Mpina ni halisi na ni kweli.

Na Sasa mtu anaweza kuanza kuamini kuwa mfumo wetu wa utawala na kikatiba ni wa hovyo sana. Hata uwe na watu wazuri na wasomi na wenye maono bora kuisogeza nchi mbele, wakiingia kwenye serikali inayosimamiwa na mfumo wa kisheria na kikatiba tulionao unaompa mamlaka ya mungu - mtu Rais wa JMT, huyo mtu hataleta impact yoyote. Atamezwa na uchafu na yeye kuchafuka vilevile.

Mfano ni Kijana Hussein Bashe. Wame - trap na amekuwa trapped kwenye tope la kashfa ya ufisadi wa Sukari!!
 
Hii nchi Ina mazezeta wengi kiasi hiki. Nadhani wewe uko kwenye top3
 
Nadhani huko aliko anajutia uamuzi wake😂
 


Kuna wakati fualani nilisikia kule Somalia. Paliwahi kuwa na gap sugar kubwa miaka fulani ya nyuma.
Ulichezwa mchezo na mafisadi wakishirikiana na watendaji wa serikali . Wakatengeneza kampuni feki isiyo na sifa ya kuagiza sukari.
Mbaya zaidi walitenga pesa nyingi za serikali . Zikalipwa ukatengemezwa mchongo ikaingizwa meli ya sukari toka Eritrea kimchongo . Imasimama kwenye bandari ya mogadishu picha zikapigwa kuwa sukari imaingizwa tani elfu 60 na ushee. Vibali feki vikatengenezwa kuonyesha kuwa mzigo umefika na kutolewa . Jambo la kusikitisha inasemekana kuwa Ile meli haikushusha mzigo wa sukari hata Tani moja . Iliondoka na mzigo wake wa sukari na kuelekea Komoro. Mchazo ukaishia hapo.
Pesa za kuagiza sukari zikapigwa sh. mil.500 za wakati huo .

Mbunge mmoja akalalamika kuwa serikali imefanya udanganyifu mkubwa lakini hakusikilizwa kutokana na bunge kuwa la chama kimoja na machawa ambao kipindi hicho waliitwa kunguni.

Tume iliundwa kuchunguza ili iweke wazi kuwa ni magodown yapi yalitumika kuhifadhi sukari iliyopakuliwa na meli kwa tarehe zilizoainishwa.
Matokeo ya tume yalibaini kuwa hapakua na magodown yalohifdhi sukari kwa tarehe hizo na wala mzigo wa sukari haukushushwa bandarini bali ni ujanja ulitumika tu.
 
Mkuu kwa wabunge hawa wa ccm hakuna ushahidi hapo ni takataka kama takataka zingine. Tunawabunge wapumvavu sana nchi hii
 
Nadhani hata hawakujitahidi kuelewa mradi ni jambo kupinga ufisadi wamekurupuka kuzima. Hii report itawarudia kama mshale ni jambo la muda tu hizo kinga zao zitatobolewa. Ni muhimu 2025 kutupa pembeni wauza bandari wote.
 
Eti kumpongeza speaker kwa uzalendo badala ya kumlaani kwa usaliti kwa umma wa wananchi. Ujinga gani huu..Japo tungekua tumeshuhudia bei ya sukari imeshuka ila yoye yamebakia mbinu za kufankisha unyonyaji mkubwa wa wafanyibiashara fisadi kwa wavuja jasho wa nchi hii
 
Wale wasiompenda Luhaga Mpina wanaumia sana sasa hivi. zitto junior Umeuona ushahidi wa Luhaga Mpina?
Usije pitwa baadaye tukaanza kulumbana kaka, pitia hapa.
Vipi mkuu una maoni gani baada ya kamati kuthibitisha Mpina ni muongo? Haaahaaa eti hajawahi shindwa thibitisha.
 
Vipi mkuu una maoni gani baada ya kamati kuthibitisha Mpina ni muongo? Haaahaaa eti hajawahi shindwa thibitisha.
Hahaha hakuna alipoongopa wamemfanyia wanavyofanya siku zote kwa wasiowataka. Mbona hili tulilijua tangu mwanzo?!, Au hufuatilii watoa mada humu, wengi tuliisha tabiria yatakayo mkuta, wala halikuushangaza umma, hiyo ndiyo ccm.
 
Usikute zile jamba jamba alizokuwa anapewa Bashe na Makonda zinahusiana na ushahidi huu wa mpina,wakaamua kumzima Makonda kwa kumshusha cheo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…