FULL TEXT: Maelezo ya Ushahidi wa Luhaga Mpina kwa Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson juu ya Waziri Hussein Bashe kusema Uongo Bungeni kuhusu Sukari

Hii kitu ya Mpina ni Ndefu sana, nimetumia akili Mnemba kupata summary:
  1. Idadi ya Tani za Gap Sugar: Waziri alidai kuwa nchi ilikuwa na gap ya tani 60,000 mwaka 2022/2023, lakini Mpina alisema ukweli ni kwamba gap ilikuwa tani 30,000 na si tani 60,000.
  2. Uingizaji wa Sukari: Waziri alisema hakuna hata kilo moja ya sukari iliyoagizwa, lakini Mpina alitoa ushahidi kwamba tani 6,801 za sukari ziliingizwa nchini.
  3. Vibali vya Kuagiza Sukari: Waziri alisema viwanda vilishindwa kuagiza tani 60,000, lakini ukweli ni kwamba viwanda vilipata vibali vya tani 12,500 tu, na muda wa vibali hivyo ulikuwa mfupi.
  4. Kanuni za NFRA: Waziri alisema kuwa Kanuni za NFRA zilibadilishwa kuruhusu kuagiza sukari, lakini Mpina alithibitisha kuwa hakuna GN yoyote iliyotungwa hadi sasa.
  5. Muda wa Kuagiza Sukari: Waziri alilalamika kwamba sukari haikuingizwa kufikia mwezi Februari, lakini Mpina alisema vibali vilitolewa mwezi Januari, na hivyo haiwezekani sukari iwe imeingizwa ndani ya wiki mbili.
  6. Uzalishaji wa Sukari: Waziri alisema viwanda vilikuwa havijaanza uzalishaji hadi Juni 4, 2024, lakini Mpina alithibitisha kwamba viwanda vilianza uzalishaji mwishoni mwa Mei na mwanzo wa Juni.
  7. Matumizi ya Sukari: Waziri alisema matumizi ya sukari kwa mwezi ni tani 45,000, lakini Mpina alisema wastani ni tani 38,000 hadi 41,000.
  8. Bei ya Sukari: Waziri alisema sukari ilifikia bei ya Shilingi 10,000 kwa kilo mwezi Januari na Februari, lakini Mpina alisema bei ilikuwa kati ya Shilingi 4,000 na 6,000 kwa kilo.
  9. Mfumo wa Usambazaji: Waziri alisema kuna msambazaji mmoja anayehudumia mikoa 11, lakini Mpina alithibitisha kuwa kila kiwanda kinao wasambazaji wake mbalimbali.
  10. Intervention ya Serikali: Waziri alisema ameitisha wazalishaji wa sukari kwa mazungumzo, lakini Mpina alisema ni wazalishaji waliomba kuonana na Waziri na walikosa mwitikio wa Waziri.
  11. Uwezo wa Viwanda: Waziri alisema taifa halina uzalishaji wa sukari kwa miezi 8, lakini Mpina alithibitisha kuwa viwanda vilikuwa vinazalisha isipokuwa kipindi kifupi cha mvua nyingi za El Nino.
 
Ingelikuwa ni nchi angalau inayokaribia kukucha, kuna watu wangekuwa wameshaitwa Kisutu long time.
Hiyo ni sukari pekee, yalifukuliwa madudu ya sekta nyingine: mafuta, umeme, . .. Dah!
 
Tuna speaker wa ajabu. Mbunge anatoa ushahidi wake tena kwa maandishi anaishia kuburuzwa kamati ya nidhamu eti kumdharau speaker. Saa ngapi wameona ushahidi wake sio sahihi maana hiyo ni njia yakumtisha mbunge. Eti ndio supika wa mabunge ya dunia. Huu mchongo mtupu.
 
Kwa jinsi ninavyozifahamu Tawala za ki-Afrika zilivyo za kidhalimu na zenye unafiki mkubwa, badala ya kumuadhibu Waziri Hussein Bashe aliyesema UONGO Bungeni ataadhibiwa Mbunge Luhaga Mpina aliyesema UKWELI.
 
Naamini wanaccm na maadui wa luhaga mpina wanachekelea kauli ya spika na bila shaka hata kamati ya maadili ya bunge ni kama imeshaambiwa Cha kufanya ! Najua kumpa adhabu mpina kutamuimalisha zaidi kuliko kumuangusha ! Namshauri mpina sasa ni mda wa kuingia jimboni kwa nguvu zote na kupiga spana za maana Kijiji kwa Kijiji, ongea kwa lugha kisesa Ina mtu kweli kweli na ulisema hujatumwa bungeni kwenda kucheza dansi na mawaziri ! Nchi imempata msema kweli mmoja tuungane kumlinda !
 
Nitawaomba chadema wamuunge mkono kwenye jimbo hilo tu!
 
Kwa sababu Jimbon kwake ndio waathirika pekee wa huu ufisadi, Nchi imejaaa wapumbavu sana hii.
 
Labda kama haujui Dola_ mpina kuzimwa ni Dakika 1 tu anajiamini sababu Rais hajatoa tamko lolote anachokifanya mpina sasa ni kumfanya Rais awe attention na suala la sukari aone namna gani Bashe anamhujumu .

Kama Rais hatatoka tamko lolote Mpina hakuna wa kumfanya yeyote Rais ndio kauli ya Mwisho Tanzania

Suala la kijiji kwa kijiji hawezi fanya bila kupewa baraka za mtu juu
 
Well said comrade
 
Aksante sana si unajua wabongo tulivyowavivu wa kusoma document kubwa tena yenye mixed scernarios na concept. Hii summary imetulia
 
Hili tatizo la sukari lipo miaka mingi sana nchini. Nakumbuka hata waziri Idi Simba lilimsumbua wakati wa Mkapa. Kuna hela nyingi sana kwenye hii kitu.

Dawa yake ni sisi wananchi kuacha kutumia sukari. Tutafute alternative yake.
Hiyo alternative nayo itatengenezewa zengwe kama ilivyo kwenye sukari
 
KWA HAYA NILIYOYASOMA BASI KUNA UCHAFU MWINGI SANA UNAENDELEA SEREKALINI URATIBIWA NA VIONGOZI AMBAO WANAJIFANYA WANAWATUMIKIA WANANCHI.
Hatua za mapema zisipochukuliwa nchi itatumbukia kwenye shimo baya sana.

Uongozi ni m-bovu sana kuanzia viongozi wa juu wa serekali.

Wakuirudisha nchi kwenye mstari ni nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…