figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
TAARIFA YA UFAFANUZI YA MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU SINTOFAHAMU INAYOENDELEA JUU YA SAKATA LA UTOAJI WA VIBALI VYA KUINGIZA SUKARI KUTOKA NJE YA NCHI NA HATMA YA KILIMO CHA ZAO LA MIWA NCHINI.
LEO TAREHE 29 JULAI 2024.
UTANGULIZI
Ndugu Waandishi wa Habari, Nianze kwa Kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa wema na fadhili zake kutuwezesha kukutana leo Tarehe 29 Julai 2024 tukiwa na afya njema na utimamu wa kuendelea kulitumikia Taifa letu la Tanzania.
Ndugu Waaandishi wa Habari, Nimewaita kuzungumza nanyi baada ya kupokea simu kutoka kwa waandishi na vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi kutaka ufafanuzi wangu kuhusu yanayoendelea kuzungumzwa kuhusiana na Wakulima wa miwa na sakata la sukari kwa ujumla wake ambalo lilianzia bungeni kwa mara ya kwanza Tarehe 4 Juni 2024 na sasa linaendelea kujadiliwa nje ya Bunge.
Mtakumbuka nilipofanya mkutano nanyi cha tarehe 29 Juni 2024 nilielezea nia yangu ya kwenda Mahakamani kutokana na sakata la utoaji holela wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi na kufungiwa kutohudhuria vikao 15 vya Bunge kuanzia Tarehe 24 Juni 2024.
Chama cha Wazalishaji Sukari Tanzania (TSPA) Tarehe 2 Julai 2024 walizungumza na waandishi wa habari kuelezea malalamiko yao ya kusingiziwa mambo ya uongo kuhusu uagizaji wa sukari nje ya nchi.
Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) nayo ikajitokeza mbele ya waandishi wa Habari tarehe 5 Julai 2024 ambapo pamoja na mambo mengine walilalamikia upotoshaji uliofanywa na baadhi ya watu kuhusu suala la uzalishaji na utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi.
Baadaye tarehe 17 Julai 2024 walijitokeza Wakulima wa Miwa kutoka Bonde la Kilombero mkoani Morogoro ambapo walizungumza na vyombo vya habari na kutoa malalamiko yao ya kukosa soko la miwa kutokana na soko la ndani kujaa sukari ya kutoka nje ya nchi na kusababisha sukari inayozalishwa nchini kukosa soko. Pia mbali na hilo Wakulima hao waliahidi kwenda Mahakamani kupinga Sheria ya Fedha ya Mwaka 2024 ambayo imefanya marekebisho ya Sheria ya Sukari bila kuwashirikisha.
Kutokana na wadau wa sekta ya sukari kutupiana mpira kuhusiana na suala la utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi na kwa kuwa kashfa hii mimi ndiye niliyeiibua Bungeni kwa mara ya kwanza, imenilazimu kutoa ufafanuzi wa baadhi ya maeneo ambayo tulianza nayo ubishani kuanzia bungeni hadi mjadala huu ulipotoka nje ya Bunge ili watanzania waujue ukweli usiotiliwa mashaka.
Pia soma:
1. Kuelekea 2025 - Luhaga Mpina amshtaki Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuondolewa Bungeni kinyume na Sheria
2. Kuelekea 2025 - Luhaga Mpina kufungua Kesi zote ndani ya masaa 24
3. FULL TEXT: Maelezo ya Ushahidi wa Luhaga Mpina kwa Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson juu ya Waziri Hussein Bashe kusema Uongo Bungeni kuhusu Sukari