Full Time: Liverpool 4 -0 Tottenham Hotspur | EFL Cup | Anfield | 06.02.2025

Full Time: Liverpool 4 -0 Tottenham Hotspur | EFL Cup | Anfield | 06.02.2025

Mboju

Member
Joined
May 4, 2021
Posts
78
Reaction score
178
Muda mchache ujao wababe wa Anfield watakuwa uwanjani kumenyana na Tottenham huku wakimkosa Trent,

BOSI wa Liverpool Arne Slot amesema beki wake wa kulia Trent Alexander-Arnold ataukosa mchezo huo wa marudiano wa nusu fainali ya Carabao Cup dhidi ya Tottenham Hotspur leo Alhamisi dimbani Anfield

Trent-Alexander Arnold alifanyiwa mabadiliko ya lazima mnamo dakika ya 70 katika mchezo wa ligi kuu waliopata ushindi wa 2-0 mbele Bournemouth Jumamosi baada ya kuumia nyama za paja

“Ataukosa mchezo huu. Tutaona kama atacheza Jumapili lakini uhakika ni kwamba hatakuwepo kesho ( leo ). Aliondoka uwanjani na maumivu lakini tayari amerudi kwenye uwanja wa mazoezi si na wachezaji bali kocha wa viungo hivyo tuwe na subira tuone ni mda gani atachukua” – Amesema Slot

Liverpool ambao wanatetea ubingwa wa kombe hilo walilotwaa wakiwa na Jurgen Klop msimu uliopita watakuwa nyumbani kusaka nafasi ya fainali huku wakiwa na kazi nyepesi ya kupindua ushindi wa 1-0 wa Tottenham katika mzunguko wa kwanza. Mchezo huo kama ule wa jana wa Arsenal na Newcastle utapigwa majira ya saa 5 usiku saa za Afrika Mashariki.

Usikose kuitazama mechi hii live muda mchache ujao kupitia simu yako download App inayoonesha mechi hii live kabisa BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP
 
Ungeweka tangazo vizur sio tunadownload tunakuta ujinga ujinga ndio maana mnaitwa matapeli
 
Back
Top Bottom