Full Time: Mwadui FC 2 - 2 Simba SC kutoka dimba la CCM Kambarage, Sinyanga

Mkuu Jose samahani kwa kukutoa nje ya mada.
Nahitaji kujiunga na Jukwa la Dini na Imani humu jamii forum, nifuate hatua zipi?
Napenda sana masuala ya Dini na Imani.
Nipe njia Mkuu niweze kuingia huko nami nifurahi.
Jaribu kuwasiliana na hawa watu...tuma maombi kwa Moderator, Invisible au Boss Maxence Mello.
 
Kudroo sio tatizo sana. Ila simba viongozi walifanya makosa sana kwenye usajili wa dirisha dogo walipaswa kuachana na mavugo na luizio na kutafuta mtu wa kumpa changamoto boko. Zaidi ya boko simba haina mshambuliaji wa kati wa maana labda kitandu yupo vizuri kiasi. Hao akina okwi, kichuya, gyan ni mawinga tu.

Makocha nao wakafanya kosa kubwa sana la kiufundI kumuingiza mavugo badala ya kitandu (dogo wa timu B). Siku zote simba inaonekana nzuri kwa sababu Boko ananza kukaba kuanzia mbele kitu ambacho mavugo hakiwezi. lakini nilimuangalia kitandu zanzibar yupo vizuri anakaba, ana nguvu, anapambana na mabeki wa timu pinzani, ana pumzi nzuri na ana kasi. ila anakosa uzoefu tu na jicho la goli vitu ambavyo vinakuja taratibu. kwa mechi ya jana kitandu angeingia baada ya boko kuumia nina hakika simba ingeshinda kwa sababu mwadui bado wangebaki kwenye goli lao lakini walikuwa wanapanda kuelekea goli la simba kwa sababu walikuwa wamebaki na mtu mmoja tu wa kumchunga naya ni Okwi basi. ni wakati sasa wa makocha kumwamini kitandu kama walivyomwamini mlipili nafikiri itwasaidia sana kuliko kumpanga luizio au mavugo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…