Fumbo: Huko Ndani Kuna Nini?


karibu tena ADii, wazo lako mwanana,
najua hukusudii, japo wakolea hina,
hisi zangu hurudii, fumbo lifanya fumbana,
majibu siyasikii, magwiji mekula kona!

fumbo si la ndoa, poswa wala kuposa,
wote mmetia doa, na jibu mmelikosa,
msichoke kuchokoa, punde jubu tanusa,
majibu siyasikii, magwiji mekula kona!

wengine wanisabahi, bila majibu kutoa,
leo ninawastahi, kesho nitawaumbua,
nangoja wazo sahihi, kama karanga chambua,
majibu siyasikii, magwiji mekula kona!

sioni hata wakongwe, wapi mekimbilia,
au wataka wahongwe, jukwaa kulirudia?
kama vipi walengwe, huko wakojichimbia
majibu siyasikii, magwiji mekula kona!
 

nimekusoma mkuu, bold nimenakili,
wanena yalo makuu, japo ni kwa ubahili,
fumbua ukae juu, kwa mwanzi we mkali,,
tupe walau nukuu, hata ikiwa mithali,

hapo bitwini dhe legs, ndipo palipo na jibu,
mwataka za nini kiss, hadi mwageuka bubu,
zaenda wapi stress, bila ya hata kutubu,
tupe walau nukuu, hata ikiwa mithali,
 

JF kuna vipaji, hongereni!
 

Yaani mkielewa hili kwahakika wala hamtajikondesha......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…