mtafuta-maisha
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 1,982
- 2,931
BTK ni kifupi cha Bind, Torture and Kill. Herufi hizi tatu zilikuwa zinawatia hofu kubwa wakazi wa Wichita, Kansas pale zilipotamkwa sehemu yoyote. Hizi herufi zilikuwa zikiwakilisha jina la mtu asiyefahamika aliyekuwa akifanya mauaji kwa miaka mingi mfululizo nanjia alizokuwa akitumia katika kuwashughulikia wahanga wake, yani aliwafunga, akawatesa sana na kasha kuwaua.
Kwa zaidi ya miaka 30 pasipo kukamatwa, BTK aliua watu 10 ampapo mtu wa kwanza alimuua mwaka 1974 na aliendelea kutekeleza mauaji mpaka alipokamatwa mwaka 2005. BTK mpaka leo anaendelea kuwa kati ya wauaji ambao walisumbua vyombo vya ulinzi vya Marekani kwa muda mrefu, na walipofanikiwa kumkamata, watu walipigwa butwaa walipofahamishawa juu ya uhalisia wa BTK.
Kwa mara ya kwanza BTK alitekeleza mauaji mwaka 197 kwa kuwaua wanafamilia wanne wafamilia ijulikanayo kama Otero. Wahanga walikuwa baba, mama na watoto wao wawili ambapo mmoja alikuwa na umri wa miaka 9 huku mwingine akiwa na miaka 11.
Watoto na baba yao waliuawa kwa kuzibwa njia za kupitisha hewa kwa kutumia mifuko ya plastiki, wakati mama yeye alikutwa ametundikwa kwenye bomba la kupitisha maji machafu. Mbaya zaidi ni mtoto wao wa tatu ajulikanaye kama Charlie ndiye alikuta maiti hizo nyumbani kwao aliporudi kutoka shule.
Baada ya miezi minne BTK alifanya mauaji tena ambapo tarehe 4, mwezi wa 4 mwaka 1974,mwanadada Kathryn Bright aliyekuwa na umri wa miaka 21, alikutwa amechomwa kisu akiwa nyumbani kwake, alikimbizwa hospitali ila kwa bahati mbaya alifariki. Baada yah iii tukio BTK alipumzika ikapita miaka mitatu pasipo kufanya mauaji mpaka aliporudi tena mwaka 1977, ambapo aliingia kwenye nyumba ya mwanamama Shirley Vian, akafungia watoto wake bafuni na kasha kumkaba mpaka alipokata roho. Mwaka huo huo aliua mwanamke mwingine, mji wa Wachita uliingiwa hofu, kila familia ilikuwa imejawa na hofu ikihofia usalama wa wanafamili.
BTK hakuishia hapo alianza kuwatumia barua za vitisho na kejeri polisi pamoja na magazeti, huku akijinasibu kwa kutekereza mauaji hayo. Yeye ndiye aliwapigia polisi kuwapa taarifa ya mauaji aliyoyatekereza mwaka huo 1977. BTK alikuwa akifurahia sana jinsi vyombo vya habari vilivayokuwa vikiandika habari zake. Kuna kipindi aliwatumia polisi mdori ambao alikuwa kaufunga na kuuvisha kama mmoja wa wahanga wake aliowaua, huku akiwaleleza kuwa huo mdori unaonyesha jinsi alivyomtesa na kumuua huyo dada, pia aliwatumia na leseni ya udereva way huyo dada.
Baada ya mauaji ya mwaka 1977, ilipita miaka minane pasipo BTK kutekereza mauaji yoyote, mpaka fununu ziliibuka kwamba huenda amefariki au alishakamatwa yuko gerezani. Mawazo haya yalifungwa tarehe @& mwezi wa 4 mwaka 19875ambapo BTK alimkaba na kumuua mwanamama Marine Hedge aliyekuwa na umri wa miaka 53. Pia aliua wanawake wawii mwaka 1986 na 1991. BTK aliwachanganya polisi maana walikuwa wakijaribu kutatua kesi ambayo haikuwa na ushahidi wala mshukiwa, kwakuwa BTK hakuacha ushahidi kabisa katikakutekereza mauaji yake japo mara nyigi alikuwa anaacha mbegu za kiume eneo la tukio lakini polisi walishindwa kujua mwenye DNA hiyo ni nani.
Mask aliyokuwa akivaa Rader wakati akitenda mauaji
JE BTK NI NANI?
Kwa kipindi chote cha mauaji hayo, kulikuwa na mwanaume aliyekuwa akiishi maisha ya kawaida kabisa kabisa hapo Wichita na alijulikana kama Dennis Rader. Radern alikuwa kaoa akiwa na watoto wawili. Alikuwa mwenyekiti wa baraza la kanisa aipokuwa akisali huku akiwa Compliance Officer wa mji aliopkuwa akiishi.
Tofauti na alivyoonekana mbele ya watu, Rader alikuwa akiishi maisha mengine ya siri ambapo alikuwa ni muaji na mtesaji mkubwa. Rader aliwapa polisi ukweli wa maisha yake ya siri alipokiri ukweli juu ya mauaji na maisha yake ya uovu aliyokuwa akiishi. Rader alianza kutamani kutesa wanawake akiwa bado kijana mdogo. Wakati huo alianza kuwa anaua wanyama. Baadaye alijiunga na jeshi la anga na kuhamia Wichita baada ya kuondolewa jeshini mwaka 1970.
Matamanio ya uovu wa Rader yalizidi kukua siku baada ya siku mpaka alipoamua kuchukua hatua mwaka 1974 pale alipoua wanafamilia wa Otero. Lakini kwa kipindi chote cha mauaji yake, Rader aliendelea kuishi maisha ya kawaida mbele ya jamii yakena alikuwa akiheshimika sana na akionekana kama mume bora na baba mwenye upendo lakini ukweli ni kwamba alikuwa na maisha yake mengine ya siri .
Mwanzoni mwa mwka wa 2005, Rader alifanya kosa kubwa sana amalo ndilo lilisababisha akamatwe, kwani huenda singelikamatwa kabisa kama asingefanya kosa hilo. Rader aliacha box dogo la nafaka kwenye pick up ya askari mmoja, na askari alipoona box hio hakulifungua akidhani kuna takataka akalitupa kwenye pipa la taka. Tofauti na matarajio ya Rader aliyekuwa akisubiri kusikia akizungumziwa kwenye magazeti baada ya askari kufungua box hilo, alipoona hakuna habari yake aliamua kupiga simu kwenye kituo kimoja cha habari akiuliza kuhusu box hilo ambalo aliliacha kwenye pick up.
Polisi waliweza kulitafuta na kulipata box hio ambalo lilikuwa limejazwa na karatasi zenye maelezo ya mauaji ambayo Rader alikuwa akipanga kutekereza mwaka huo. Pia kulikuwa na swali alilowauliza na swali lenyewe lilikuwa kama anaweza wasiliana na polisi kupitia floppy disk. Pia aliwataka polisi kuwa wakweli kama akitumia floppy hawataweza kumkamata na aliwataka kama jibu ni ndiyo wamjibu kupitia gazeti la mji huo kwa kuweka tangazo flani.
Polisi walihisi hii ndiyo nafasi pekee inayoweza kuwasaidia kumkamata mhalifu huyu, hivyo waliweka tangazo kama alivyowataka ambalo yeye alipolisoma alielewa kuwa hawezai kumpata kupitia floppy disk, jambo hili halikuwa kweli.
Tarehe 16, mweiz wa 2 mwaka 2005, Rader alituma floppy disk kwenda kwenye kituo kimoja cha habari. Kwa kuchuguza hiyo Floppy Disk wataalamu wa kompyuta wa jesi la polisi waliweza kugundua kwamba file lililomo kwenye hiyo floppy disk limehifadhiwana mtu ajulikanaye kama Dennis, na hiyon Floppy iliwahi kutumika katika kanisa la Christ Lutheran na pia iliwahi kutumika katika Library ya City Park. Katiak uchunguzi wao polisi waligundua kwamba kulikuwa na mtu ajulikanaye kama Dennis Rader aliyekuwa rais wa wanakongamano wa kanisa la Christ Lutheran na alikuwa akiishi katika mji mdogo wa Park.
Polisi wakaanza mchunguza Dennis Rader, na wakaanza kuchunguza DNA yake walizokusanya kutokana na mbegu alizokuwa akiacha kwenye maeneo aliyotekeleza mauai yake kwa kuioanisha na DNA ya mtoto wake wa kike ambayo polisi walifanikiwa kuipata pasipo Radaer kujua. Majibu yalipokuja DNA zilishabihiana kwa asilimia mia. Dennnis Rader alikamatwa tarehe 25 mwezi 2 mwaka 2005. Kwenye mahojiano inasemekana kwamba Rader alikasirishwa na kushangazwa imekuaje polisi walimuongopea kwamba hawawezi kumfuatilia kupitia floppy disk. Alidai hakutegemea kama chombo kikuwa kama polisi kingeweza kusema uongo.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake tarehe 27, mwezi wa 6 mwaka 2005, Rader aliielezea mahakama jinsi alivyotekereza mauaji yote kwa ukamilifu.. dennis Rader alipewa adhabu ya vifungo 10 vya maisha , kila kimoja kikiwa adhabu ya mhanga mmoja.