Fungua karakana ya kuongeza thamani kwa vitu vilivyotumika

Fungua karakana ya kuongeza thamani kwa vitu vilivyotumika

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Kwa leo nitaongelea viatu 'used'/mtumba

Kuna siku nilitembelea duka moja la viatu vya mtumba mkoani Arusha; hivyo viatu vilikuwa vinatoka Italy, kuuliza bei, naambiwa sh. 185,000/=.

Hapo nikawa nimepata wazo la kiujasiriamali kichwani:-

Utaanzaje sasa:-​
  • Nunua mashine ya kushonea viatu​
  • Tafuta jengo/fremu/ofisi​
  • Tafuta fundi wa kushona viatu; unaweza kumtoa huko kijijini na kumleta mjini​
  • Nenda kwenye viatu vya mtumba ukanunue kwa jumla​
  • Vilete kwenye karakana yako, na uviongezee thamani​
  • Kama vimechanika, vishone​
  • Vioshe​
  • Ving'arishe​
  • Badilisha au boresha soli iliyopo​
  • Kinyooshe vizuri​
  • Peleka sokoni​
  • Kwa makadirio; kwa bei ya jumla utakuwa umenunua kwa 15,000, baada ya kukiongezea thamani, uza 45,000 au zaidi.​
Aya ingia kazini, acha kulalamika​
 
Mimi nimeona akina mama wa Kimasai wakisindika ngozi za mbuzi na kondoo halafu wanashona pochi, mikoba, sandles n.k ila sioni wakipiga hatua sasa sijui hailipi au mbinu za kibiashara si sahihi.
 
Mi nimeona aki na mama wa kimasai wakisindika ngozi za mbuzi na kondoo halafu wanashona pochi, mikoba, sandles n.k ila sioni wakipiga hatua sasa sijui hailipi au mbinu za kibiashara si sahihi
Ukiwatumia vizuri, unaweza ukatajirika:-
  • Thaminisha ubora wa bidhaa zao​
  • Wape oda wakutengenezee wewe kwa wingi kama mtaji unao​
  • Fungua kampuni i.e mx exporters n.k​
  • Tafuta masoko ya ndani na ya nje; hapa tumia nguvu nyingi​
  • Pokea pesa​
 
Hii idea ungeiweka katika furnitures used kama viti, makabati, vitanda na meza itapendeza zaidi. Ingawa utahitaji mtaji kiasi ila ni biashara nzuri.
 
Hii idea ungeiweka katika furnitures used kama viti, makabati, vitanda na meza itapendeza zaidi. Ingawa utahitaji mtaji kiasi ila ni biashara nzuri
Ni wazo zuri pia
 
Hii idea ungeiweka katika furnitures used kama viti, makabati, vitanda na meza itapendeza zaidi. Ingawa utahitaji mtaji kiasi ila ni biashara nzuri.
100%[emoji106]Kuna wahindi fulani nimewaona wanaifanya hii wanapiga hela,vile vitu vinang'arishwa huwezi kujua kama ni used akienda mteja mshambamshamba anaambiwa ni vipya analipia mpunga.
 
Kuna jamaaangu yeye ana kibanda tu kakizungushia mabati kipo pembeni tu ya barabara

Juu ya kibanda kaandika TUNANUNUA NA KUUZA VITU USED, ina maana hata kitanda au makochi yeye ananunua kwa gharama ndogo.

Anachokifanya sasa[emoji16][emoji16][emoji16]

Anachukua kitanda anakufumua au kukipiga msasa kinakuwa kikali balaa, yaani ukipota pale lazima utajuta kama ulimuuzia.

Then anauza
 
Ushamba wenu wa Arusha msiulete dar na pwani sasa kiatu 185k vingapi pale karume ni mpaka 20 vikali ndo vinauzwa huko mpaka laki 2

Ishu ni furniture kwa maeneo kama dar ndo wanapiga pesa sio midosho kwa dar na maeneo kibao Haina thamani
 
Back
Top Bottom