VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilianza na inaendelea na uchunguzi wa sakata la rushwa kubwa ya mabilioni dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Hii ilifuatia agizo lako kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza mkataba tata wa vifaa vya jeshi hilo uliosainiwa. TAKUKURU wakajipanga na kuanza kazi. Kazi inaendelea.
Ni hivi juzi tu 'umetoa msamaha' kwa makamanda wa Jeshi hilo la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na aliyekuwa Mkuu wao Kamishna Thobias Andengenye. Hadi sasa, Rais na Mwenyekiti wangu haukusema kama Lugola naye amesamehewa. Mkuu wetu wa Serikali na chama, tuweke wazi kuhusu mambo haya. Je, msamaha ulioutoa unahusu hadi uchunguzi uliokuwa ukifanywa na TAKUKURU dhidi ya Makamanda hao? Na je, TAKUKURU wachane na kutokomeza makabrasha ya uchunguzi wao huo?
Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM, kumbuka kuwa sera ya kupambana na ufisadi na wizi ndiyo iliyokubeba mwaka 2015. Mwaka huu vipi hadi 'uigaragaze' katika dakika hizi za lala salama?
CCM tunataka tarehe ya kuchukua fomu ya Urais ili wenye uwezo wajitokeze, utaratibu hauzidi Katiba yetu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dodoma