Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,395
- 2,391
Kwanza kabisa kuacha mazoea fulani katika maisha yako si rahisi kama unavyotamka,unaweza kuacha leo lakini ikachukua muda kuacha kabisa.
Leo karibu marika yote na jinsia zote katika jamii ni waraibu wa kamari. Uraibu huu unatokana na matangazo ya kuvutia na zawadi kubwa kubwa pia ile imani kuwa "ipo siku moja tu" yani atafanikiwa kupata pesa nyingi kwa dau kidogo. Kivutio cha michezo hii ni matangazo ya kibiashara pamoja na zawadi zinazotangazwa mitandaoni na kokote. Matangazo hayo yanashawishi sana na wewe kuanza kutafuta pesa kwa njia hiyo.
Michezo ya kamari ipo mingi sana, kubet,kucheza karata za pesa,pool table,dubuli(bonanza) keno, mbwa .n.k lakini mimi nilikuwa mraibu wa kubet hasa mpira wa miguu ndio nitakaozungumzia sana japo hata waraibu wa michezo mingine mnaweza kufuata hatua zangu.
Katika kubet balaa linaanza unapokula au unapoona mtu kala basi unaamini na wewe una haki ya kula au ipo siku utakula na wewe. Siku ukila hata kama ni pesa ndogo tu unajiona wewe ndio mjuaji wa kubet,wewe ndio bosi siku hiyo,unaweza hata kupanda boda umbali wa m200 tu,au hata kumtukana mtu,pesa ya kubet ina jeuri sana.
Nilianza kubet mwaka 2013 kipindi ambacho alikuwa ameshika soko ni muhindi. Baadae ikaja meridian.
Haraka nikahamia meridian sababu kuu nilikuwa na uwezo wa kucheza online na maduka yake yalikuwa ya ndani sio sehemu za wazi kama kwa muhindi.
Kitendo cha kucheza online kilifanya nitumie muda mwingi sana kwenye simu sababu kuna kuangalia fixture(ratiba ya michezo) kuangalia ratiba ya game za leo na kuweka dau.
URAIBU ULOVYOANZA
Kwenye simu unatakiwa kuwa na Apps au kuwa online kwenye website zaidi ya tatu kwa wakati mmoja.
Kwenye kamari kwenyewe, kwenye app ya kuchambua huo mchezo pamoja na web ya kufuatilia huo mchezo kama utacheza "In play" na kwenye makundi yenu.
Kutokana na muda huo hutopata muda wa kuweka sinu chini hata kama unangea na mtu.
MADHARA YAKE
Nilicheza kawaida na online pia, online michezo aina zote live na kawaida. Kamari ilifanya nione watu wengine kama mzigo hawana umuhimu tena,mimi na simu tu,nikitoka kazini najifungia ndani mpaka saa 3 usiku natoka naenda kula huku nikiwa na simu.
Hata ukikutana na rafiki yako huwezi kuongea nae muda mrefu sababu anakuchelewesha kuweka mzigo au kufatilia game live. kutokana na umahiri wangu wa kucheza live nilipewa jina la "mzee wa in play" uraibu ukikolea mikopo isiyo ya lazima pia ikuhusu
Tulifungua group la watu wa5 wasap kwa ajili ya kupeana dili(game zenye hela) nnilikuwa silali.
Mchana nipo kazini nabet,jioni nyumbani nabet usiku online (saa 8 Usiku mpaka saa 11 asubuhi bara za Amerika kusini kuna mechi zinaendelea)hakuna kulala labda uegeshe tu.
Kama una mke mnaweza kugombana au kuleta mgogoro kama hajui wewe unabet(sababu ya muda wako kwake), hata mapenzi kwenye nyumba yako unaweza kushindwa kufanya kwa ufanisi sababu ya akili kuwa kwenye kamari tu. Yaani huna muda na mke au familia kwa ujumla,ni wewe na kamari tu.
Madhara ya kiafya yatokanayo na michezo ya kubashiri
( SOMA HAPO ☝️ muhimu sana)
Japo nilikuwa napata pesa na kuliwa pia lakini kamari ilinitenganisha sana na watu,ilifika hatua ukiwa na kiasi chochote cha pesa unawaza kubet tu,ukilala usiku unawaza na kuota mikeka tu. Ukiwa kazini unawaza kupata muda mwingi kubet,unaona kama kazi inakubana.
Mwaka 2016 nilipiga sana hela kwenye Euro2016 mpaka tukaanza kukopeshana mitaji ya kubetia.
Jinsi uraibu wa kamari ulivyomaliza maisha ya binti huyu - BBC News Swahili
2017 SAFARI YA KUACHA KUBET YAANZA RASMI
Nilianza kujifunza biblia baada ya kuda nikagundua madhara ya kamari,nikapigia taarifa nyingi na magazeti madhara ambayo waraibu wa kamari walipata nikajichunguza kweli nilivyokuwa naishi ni tofauti kabisa. Nilikua tayari kukopa pesa m-pawa ili tu nibet,huwezi kuwa na akiba kama huna pesa ya kubetia. Ukipata pesa lazma 40% irudi kubet,40% kujipongeza na 20% akiba.
maswalijuuyauislamu.com
HATUA NILIZOCHUKUA
1. Nilijichunguza mwenyewe jinsi ninavyoishi na watu
2. . Nikaangalia grafu yangu ya pesa
3. Nikaangalia muda wangu kwa siku nzima
Nikaona vyote hapo haviendi sawa kutokana na kamari
Nikaacha rasmi lakini nilitumia zaidi ya miezi 10 kutojihusisha kabisa na kamari.
KAMA UMEATHIRIKA FANYA HIVI:
Usisikilize shuhuda za wanaokula na kukutambia.
https://www.jw.org/sw/maktaba/magazeti/g201503/biblia-inasema-kucheza-kamari-ni-dhambi/
Pia unaweza kumwomba Mungu wako akusaidie kushinda vikwazo vyovyote mbele yako pia. Nimeandika kwa lengo la kusaidia jamii kwa ujumla sababu kuna wengine wanatamani kuacha lakini hawajui sababu au jinsi ya kuacha.
Karibu kwa usomaji.

Ni yapi madhara ya Kamari na kwanini imekatazwa (haram)? | Maswali juu ya Uislamu
Elmalılı Hamdi Yazır anaeleza yafuatayo kuhusu kukatazwa na madhara ya Kamari wakati akiitafsiri aya ya 219 katika Suratul-Baqara:
HATUA NILIZOCHUKUA
1. Nilijichunguza mwenyewe jinsi ninavyoishi na watu
2. . Nikaangalia grafu yangu ya pesa
3. Nikaangalia muda wangu kwa siku nzima
Nikaona vyote hapo haviendi sawa kutokana na kamari
Nikaacha rasmi lakini nilitumia zaidi ya miezi 10 kutojihusisha kabisa na kamari.
KAMA UMEATHIRIKA FANYA HIVI:
- Usiangalie ratiba ya mipira yeyote kwa muda kama wa mwezi hivi.
- Angalia mambo uliyofanya baada kucheza kamari.
- Futa apps zote za kuangalia matokeo ya mpira(livescore,flashscore n.k)
- Usiangalie fixture popote, online au ubaoni
- Toka kwenye makundi yote ya wafuasi wa kamari

Upvote
14