Fupa la umeme kumchafua Dotto Biteko?

Mkuu ulikuwa unakatika kama kawaida, usitufanye kama hatukuwepo kipindi hiko! Mwaka 2017 kulikuwepo mgao wa umeme!

Mkuu kisa cha kuondolewa ndugu Mramba ni kukatika umeme!
 
Anaweza kuchafuka sawa, lakini Makamba ndio chanzo cha matatizo ya umeme nchini. Baada ya kuonekana HAWEZI kulimaliza tatizo ndio akaondolewa. Mh. Dotto Biteko atakuwa "bangusilo"!
Mkuu acha kupotosha, sio kweli hata kidogo. Matatizo ya umeme nchi Tanzania yapo kabla hata Makamba hajazaliwa.

Mkuu Makamba Kawa waziri wa nishati kwa miaka 2 tu, iweje awe chanzo cha matatizo ya umeme yaliyodumu kwa miaka 62?

Hata kama ni chuki, hii imezidi, imevuka mipaka!
 
Hii nchi kama mamlaka za teuzi zitakuwa zinawasikiliza watu wenye chuki binafsi tutawapoteza watu wa maana Sana katika maendeleo ya nchi yetu.

Tuache siasa za chuki tutalikwamisha taifa hili na kuwapoteza watendaji wa maana kwa maslahi ya nchi.
 
Hii nchi kama mamlaka za teuzi zitakuwa zinawasikiliza watu wenye chuki binafsi tutawapoteza watu wa maana Sana katika maendeleo ya nchi yetu.

Tuache siasa za chuki tutalikwamisha taifa hili na kuwapoteza watendaji wa maana kwa maslahi ya nchi.
Mkuu kwa tafsiri yako wenye chuki ni watu wa aina gani?
 
Kama halikumchafua januari mpaka akatolewa hapo na kupelekwa mambo ya nje basi hata Mh Biteko halitamchafua baada ya Unaibu Waziri Mkuu ndio Waziri Mkuu ajae 2025 mark my words
 
Nyuso zimewashuka hawana cha kusema, maana mvua zinanyesha mpk milima inaporomoka lkn mgawo unaendelea. Dotto Biteko bure kabisa huyu.

Eti mwalimu wa primary anakuwa naibu waziri mkuu. Puaaa!
🤪🤪🤪🤪🧑‍🦯
 
Kwani ni lini aliwahi kuwa msafi?
 
Katika hao wote Le Profeseri Muhongo alitatua kero ya kukatika umeme ovyo na kuchelewa kupata huduma toka watu wa dharula wa TANESCO.
Mvurugano ukaanza kwa Kalemani akaja kuvuruga kila kitu Januari Makamba.
Ndani ya ccm hakuna mtendaji anaye wajali wahitaji wa huduma
 
Ni ngumu kujudge uwezo wa dereva ukimpa gari bovu, matairi hayana upepo, engine inazima kila dk 5, steering wheel haiendi unakoipeleka, mafuta hayatoshi etc. Kifupi, kwa deficiencies za grid yetu (kuanzia kwenye generation hadi kwa mtu wa mwisho) sio rahisi kujua shida ni ya dereva/waziri au ya infastructure and climate.

Hizi tuhuma za kila waziri wa nishati kuwa ame-underperform ni kupiga ramli tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…