Muziki wa Bongo unaendelea kukua siku hadi
siku na kutambulika kimataifa, kutokana na kazi
za wasanii wetu kuendelea kushika chati
mbalimbali kwenye vituo vikubwa vya kimataifa
hadi kufika nafasi za juu.
MTV Base wana chati ya video 10 za Afrika
iitwayo Official African Chart, na miongoni mwa
video zilipo katika chati hiyo wiki hii, 4 ni za
wasanii wa Tanzania.
Producer Nahreel ana kila sababu ya kufurahia
mafanikio hayo kama Mtanzania, lakini anayo
sababu nyingine ya kutabasabu kwasababu
wimbo wao Game ni miongini mwa video bora
10 Afrika kwa sasa, na anayo sababu ya ziada ya
kujivunia kwasababu yeye ndiye producer
aliyetengeneza nyimbo zote nne za wasanii wa
Tanzania zilizoko kwenye chati hiyo.
Hizi ni nyimbo 4 zilizoko kwenye African Chart
Top10 ya MTV Base wiki hii:
Nafasi ya 1 imekamatwa na diamond ft. Flavour
wimbo ni Nana
Nafasi ya 5 imekamatwa na Navy Kenzo ft.
Vanessa Mdee wimbo ni Game
Nafasi ya 7 ni Joh Makini ft. G-Nako wimbo ni
Nusu Nusu
Na Bonus track ni video mpya ya Jux ft. Joh
Makini wimbo ni Looking For You
Nahreel amezungumza na Bongo5 na kuelezea
furaha aliyonayo kwa mafanikio hayo;
Kwakweli najisikia vizuri sana, kwanza
inaniongezea nguvu ya kuendelea kufanya kazi
zaidi, kwasababu nguvu nayoiweka ni kubwa na
unajua unapoweka nguvu halafu unaona matunda
yake inakupa nguvu sana tutaendelea kuweka
juhudi mpaka hapo tutakapohakikisha MTV nzima
kuna nyimbo 10 za Tanzania. Alimaliza
Nahreel.
BY : Bongo5

Last edited by a moderator: