Ijapokuwa nipo nje ya tarehe
Namshukuru Muumba kwa kunifikisha kutimiza mwaka mwengine tena wa kusherehekea kuongeza umri niloishi hapa duniani nikiwa na siha na afya njema, kwani ni Muumba pekee ndio muweza wa kila kitu. Wengi walitamani nao waongeze umri walioishi hapa duniani ila Muumba hakujaalia hivyo. Shukrani za pekee kwa wazazi wangu kwa kunilea kwenye malezi mazuri hadi kufikia hapa nilipo, Namuomba Mwenyezi Mungu awalipe ujira ulio bora wazazi wangu kwa yale waliyopitia katika malezi yangu. Awajaalie kauli thabit Baba yangu, ndugu, jamaa na marafiki waliokwishatangulia mbele ya haki na amjaalie umri mrefu mama yangu, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki. Atuepushie kila yenye shari na atujaalie kila yenye kheri. Alhamdulillah.
Mwaka huu wakati tarehe ya kuzaliwa kwangu inatimia, bahati nzuri nilikuwa safarini.