Furaha ya Wana Simba sc itarejea endapo kamati ya usajili itagusa maeneo haya.

Furaha ya Wana Simba sc itarejea endapo kamati ya usajili itagusa maeneo haya.

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
1.kipa hii ni angle muhimu sana kwa pale simba asajiliwe kipa mwenye uwezo na wa kimataifa ikiwezekana alete competition kubwa kwa Aish manula, kwa Sasa Simba sc inamtegemea kipa Ally Salum ambaye ni kipa namba mbili Hana experience na Kama akiendelea kuaminiwa basi asitokee MTU wa kumlaumu.

2.Beki namba 2&3 kwa Sasa hizi namba zinachezwa na shomari kapombe na mohammedi husein, endapo Hawa wachezaji wakiumia Simba sc huwa wanatapa tapa Bora kwa beki namba mbili kapombe huwa Kuna msaidizi Israel mwenda kwa namna fulani Kuna umuhimu mkubwa mno kuongeza silaha za kazi haswa beki namba tatu kwa upande wa mohammedi husein.

3.beki wa Kati kutokana na makosa yaliyojitokeza na kelele za mashabiki zilizomfanya onyango aombe kuondoka, basi ipo haja kubwa kutafutwa pacha wa inonga yaani beki kitasa mwenye ability kubwa kuliko hata Onyango.

4.Winga wa kushoto (namba kumi na moja) kamati ya usaji Simba inapaswa kusajili winga wa kushoto, winga mbunifu winga mwenye akili kubwa na kasi Tena wa kitaifa.
Robertinho alikua ana mtumia sakho, muda mwingine alikaa chama lakini kiuhalisia sakho ni namba Saba na chama ni namba kumi halisi kwa hiyo bado Kuna gap kubwa hapo namba kumi na moja.

5. Kamati ya usajili iguse namba 6,8 hapa Kuna umuhimu mkubwa sana sadio na muzamiru wanahitaji watu wa mpira watakao fiti mpaka kwenye mechi za kimataifa ipo haja kamati ya usajili ipaangalie hapa katikati.

6.Jean baleke anafaa kucheza namba tisa lakini siyo mbaya kuletwa mbadala wake mzawa au wa kimataifa hakika italeta matunda makubwa.

7.asajiliwe namba kumi wa kimataifa chama ameshachoka na siyo mbunifu katika mechi za kimataifa haswa mechi za ugenini, hii ni sehemu muhimu sana.

Sakho akicheza namba Saba na kibu Denis hiyo namba inawafaa sana kwa hiyo sioni haja ya kufanya usajili kwa upande wa namba Saba.

NB: benchi la ufundi lisikilizwe na lisipangiwe Nini chakufanya, kocha apewe mamlaka atumie taaluma yake.

Endapo kamati ya usajili itagusa hayo maeneo hakika Simba sc itarejesha furaha ya mashabiki wake.
 
Simba nguvu moja! Wasipokuwa makini, miaka 10 itapita bila ya kupata hata kikombe cha maji ya kunywa.

Kila mwisho wa msimu kazi yao kubwa itakuwa ni kujenga tu timu.
 
Tunahitaji beki kitasa
Tunahitaji kiungo mkabaji asili (sio no 8 kama kanoute na mzamiru namaanaaisha no 6 ambaye hana tamaa aaya kwenda mbele kazi yake kulinda mabeki)
 
Tunahitaji beki kitasa
Tunahitaji kiungo mkabaji asili (sio no 8 kama kanoute na mzamiru namaanaaisha no 6 ambaye hana tamaa aaya kwenda mbele kazi yake kulinda mabeki)
RICHARD BOADU AGADAS - ASANTE KOTOKA - GHANA. Hapa Simba waache ubahili watoe mtonyo.
 
4.Winga wa kushoto (namba kumi na moja) kamati ya usaji Simba inapaswa kusajili winga wa kushoto, winga mbunifu winga mwenye akili kubwa na kasi Tena wa kitaifa.
Luis Miquisone

Akikosekana Simba waende kwa Camilo Bito - De Agosto Angola hawatajuta kwa huyu bwana mdogo kwani Miguisone mtupu
 
Kama Simba wanampango wa kumsajili Martin Kiiza nawashauri kabla ya kufanya hivyo watume team ya "scouting" kama wanayo iende Angola ikamtazame Camilo Bito halafu walinganishe shughuli yake na ya Martin Kiiza ndipo wafanye maamuzi. Au hata Mohamed Hussein na Kapombe wanaweza kuwashauri viongozi wao maana wameshakutana na huyu dogo kwenye mechi mbili za CAF.
 
Back
Top Bottom