Pole sana dada nakumbuka nilivokua o level kule iringa kulikua na rafiki yetu anatatizo kama lako,tulikaa na washkaji ili tuone jinsi ya kumsaidia kweli tulifanikiwa kwan tulikubaliana tuwe tunamwamsha kukojoa usiku pale tu mtu unapokumbuka hivyo tulifanya hivyo hata kama alikua ammeamshwa dakika 5 au 2 na tulimsimamia hadi akojoe, yaani jamaa alikua mtata kuamka ila tuliweza kwani mwisho wa siku ile sumbua sumbua ilimwingia akilini akazoa kwa miezi 3 tu hadi leo jamaa yupo chuo anatushukuru sana kwani anasema nyumbani hadi alitengwa kutokana na tatizo lake na alipona tukiwa form 3.
USHAURI WANGU KAMA HUNA MTU WA KUKWAMSHA USIKU KILA MARA ILI UKAJISAISIE HEBU TEGESHA ALARM KILA BAADA YA DK KADHAA ILI UWE UNASHTUKA KWENDA KUJISAIDIA THEN WAONE MADOKTA NA YOTE TISA KUMI NENDA KWENYE MAOMBI KAFANYIWE MAOMBI LABDA KUNA MKONO WA MTU ULIFANYA KOSA KUBWA KWENDA KWA WAGANGA WA KIENYEJI HATA KAMA DINI YAKO HIRUHUSU WE NENDA KWA MAOMBI DADA KWENYE KUTAFUTA TIBA HAKUNA KUOGOPA MIFANO TUNAYO!
AMANI YA BWANA IWE NAWE...
Pole sana.... Dnt feel kua dats the end for u... Kaza buti, cku moja yote haya yatakua historia, Ill pray for u, have faith and pray to God even harder.... Trust in him, Tatizo hilo litaisha sista... Much love, ......
Natumai wengi wenu mmelala kwa kua ni ucku mkubwa,bat kwa upande wangu naic ni mchana kwani ndio natoka kufua now nguo zangu,sitoweza kukufuru na mshkuru MUNGU sana na nautumikia mtihani wake alonipa,siwezi jua kipi ameniandalia kizuri kwenye dunia au akhera yangu(maisha baada ya kifo)kwani nabii Ayubu aliumwa kwa miaka mingi mpaka mke na familia yake ikamtenga na wala hakukufuru na zawadi yake kupitia mtihani wa maradhi mungu alim2nukia pepo wakati kuna walopata uzima duniani wakamsahau mungu wakaonja moto,nachotaka kusema mtihani wowote unakufanya uwe karibu na mungu wako,uwe mtihani wa maradhi,riziki,ndoa n.k,naitaji dua zenu wana jf kwani nimemaliza waganga na wagaguzi,hospital bila mafanikio,hapa nilipo mikono inauma kwakufua kila siku,mda huu na kiu lakini nashindwa kunywa maji kwasasa np macho ila nikifumbatu jicho haja ndogo inanitoka bila hisia,ila nikilala mchana wala hii hali hijitokezi ni ucku tu,nashkuru mungu ni mzuri wa sura kiasi changu nilicho jaaliwa wengi wananitaka kwa ndoa ila na sita kwasababu ya tatizo langu huenda kilio kikazidi katika ndoa,nilijaribu kueka post yangu ya kutafuta mwenza mwenye sifa kama zangu bila mafanikio,hua naumia sana ndugu na majirani kujua matatizo yangu na kunibeza mda mwengine hua nahic nawatia aibu wazazi wangu,hua nasubiri watu wote walale ndionifue naona haya kuanika kwenye kamba kwa kuepusha maswali kwanini kilasiku nafua?nguo na anika ndani kwa hiyo hukauka bila kupigwa najua kwa hali hiyo kila cku na nusurika kunga'twa na tandu au nnge hufuata ubaridi katika nguo,ebu vuta picha kipindi hiki cha kipupwe âlafu unaamka ukiwa umeroa unaskia baridi kiasi gani?na nakoga sa 11 kabla watu hawajaamka hua baridi mda huo sana naomba mungu niepushe na nimonia.Wana jf mshukuruni mungu kwa maneno na vitendo kwa neema ya uhai,uzima,rizki,mali,watoto,ndoa,n.k kuna watu hawana.ucku mwema!
Nachojua na kuamini na mie huu ni wakati wako wa KUOKOLEWA na we kupata SHUHUDA za kuwaambia watu juu ya UPONYAJI wako. Sehemu fulani ya maelezo yako yanaonesha wazi huamini wala kuabudu katika jina la YESU: ila sikia dadangu hautapata kupona sehemu nyingine yeyote isipokuwa kwa jina la YESU, nakuonea wivu kwani naona kabisa Mungu amekuchagua wewe kuwa MKOMBOZI kwa nyumba yako kupitia jina lake YESU kristo. chukua hatua sasa dadangu tafuta kanisa lolote la KIROHO ambapo kristo huubiliwa katika kweli yote. Hata sasa nakuona umepona ukianza hata kujifunza kulitamka jina la YESU. Mwite Yesu yeye ni zaidi ya yote nakwambia
Pole saan dada yangu, nami pia nilikuwa na tatizo kama hilo, nilikojoa kitandani mpaka nikiwa kidato cha pili na tatu, lakini kilicho nisaidia saana ni juhudi za rafiki zangu kunisaidia kuamka kila baada ya muda mfupi mpaka nikazoea (kitabiu inaitwa condition reflex) na pia nilipunguza kufanya mazoezi hasa baada ya masomo hili nisichoke saana na kulala moja kwa moja wakati wa usiku.
Nilionanlo kwako: tatizo hili have affected you emotionally and psychologically plus unemployment, these 3 problems are the main issues affecting your social and economic life. Je huko tayari kumuona daktari wa magonjwa ya akili
(Psychiatry, simahamishi kwamba una ugonjwa wa akili), I see you need psychocounselling to over come the problem. Are you ready for me to connect you to my friend and co-worker in the department of Psychiatry to assist you for this? Let me know, send e-mail in my JF account
MUNGU ninae mwammini atajibu haja ya moyo wako kwa kua kilio chako kimefika juu, na tujifunze kushukuru kwa kila jambo, nakutia moyo ndugu yangu, MWAMINI MUNGU tu usiende kwa mganga nenda kwa madaktari wanaweza kukusaidia kwa uweza wa MUNGU, kumbuka wapo walioishi na ukoma na kutengwa na jamii zao (kipindi hicho ukoma haukuwa na dawa) na hasa ndio source ya wimbo wa Tenzi uitwao KAA NAMI Ni Usiku tena, baada ya ndugu zake kumtenga na kumuacha porini ili ajifie kila siku aliimba wimbo huo na mstari mojawapo katika wimbo huo ulikua ukisemaKIFO NA KABURI HAVIUMI, sasa the same kwako Dada yangu, kwa kipindi hiki kaza moyo wako kwa MUNGU hebu fumba macho vuta hisia na kumbuka Mama yule kwenye Biblia alietokwa na damu kwa zaidi ya miaka 25, unafikiri alikua katika hali gani? Nawe yawezekana dada yakawa historia hayo. Simama kwa MUNGU tu, mkumbushe mkajadiliane, aitimize haja ya Moyo wako.