Furniture nyingi siku hizi ni Mchina, watu wanadanganywa Mbao ngumu

Pantomath

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
842
Reaction score
3,449
Unakuta Showcase nzuriii, inavutia ukimuliza fundi hii ni mbao ya mti gani? Anakuambia Mbao ngumu, kumbe ni haya ma play wood na sijui MBF.

Unafika nyumbani jichanganye likae sehemu yenye maji sasa. Kila siku utaishia kufagia mapumba. Kwa wale wapangaji wenzangu wa kuhama hama, kadiri unavyolisumbua ndio linakufia

.

Ni mafundi wachache sana wenye uwezo wa kufanya finishing nzuri ya mbao ionekane kama hizo play wood hapo.

Sikuhizi mpaka majeneza kwa wenzangu wakristo yamejaa ya mchina ndugu yako anaenda kuliwa na siafu tuu huko chini.

Mbao itabaki kua mbao tuu

 
Nashindwa kuelewa, watu wananunua kwa kutojua, au wanajua? Na kama wanajua wanaelewa life span yake?

Siwezi nunua furniture yoyote ya play wood, na ukifika kwa wale wanaojua kuzipekecha, wakijua wana kasirika.
Haya kimbembe kinaanza kwenye kulifikisha nyumbani tuu,
Unafika ni lakuegesha,

Baada ya hapo umewasogezea panya geto/mkate, baada ya hapo angle/edges zinaanza kulika, layer inatoka...
 
Siku moja nilikuwa napiga stories na washikaji zangu mchwa na panyaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Wote, walinihakikishia kuwa hizo fenicha za plywood board na mdf (medium density fibreboard) ni tamu sanaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ na ni mbovu zikigusa maji.
 
Ni muda wa kumuita fundi nyumbani na mbao zangu 😳😳😳
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…