Fursa: Habari Njema kutoka CRDB Benki

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Benki ya CRDB inatambulika kama kinara wa uanzishaji wa huduma na bidhaa mpya sokoni ambazo hukidhi matakwa ya wateja.
Katika kudhihirisha hilo, sambamba na kuzingatia uhitaji mkubwa wa makazi bora hapa nchini, Benki ya CRDB sasa imeleta bidhaa mpya sokoni ijulikanayo kwa jila la Jijenge . Jijenge ni mkopo wa nyumba ambao unakuwezesha wewe mteja wa Benki kumiliki nyumba ya ndoto yako kwa kununua, kujenga au kuboresha nyumba ya zamani. Mkopo huu ni sawa na kuwa kwenye nyumba ya kupanga huku ukiinuunua taratibu kila ufanyapo marejesho ya kila mwezi.
Huu ni mkopo wa muda mrefu wenye kipindi cha marejesho cha hadi miaka 20 ambao dhamana yake ni nyumba hiyo hiyo ijegwayo , iliyonunuliwa au kukarabatiwa. Kupitia mkopo wa Jijenge , wewe mteja wetu unaweza kupata hadi shilingi milioni 500 na kurejesha kidogo kidogo kila mwezi au kwa agizo maalumu kwa Benki (standing order) au kwa mkupuo na tena kwa riba nafuu ambayo ni chini ya riba ya soko.
Kwa kuwa mkopo huo ni wa kutosheleza, unakupa fursa wewe mteja kuweza kumiliki nyumba ya ndoto yako katika kipindi kifupi pasipo kusubiri kuweka akiba yako kwa muda mrefu.
Mkopo huu hutolewa kwa watanzania walioajiriwa na waliojiajiri ndani na nje ya nchi (kwa walio nje ya nchi wanapaswa kuwa na akaunti ya Tanzanite kutoka Benki ya CRDB ) na wenye umri kati ya miaka 21 hadi 60. Sambamba na hilo mkopo huu una bima ya mkopo (credit insurance) kwa mteja kama atapatwa na kifo au ulemavu wa kudumu ambao utamfanya ashindwe kuendelea na shughuli za kumpatia kipato na pia nyumba ijengwayo, inunuliwayo au kukarabatiwa huwekewa bima (property insurance) endapo itakumbwa na majanga kama vile moto na mengineyo. Kwa maelekezo zaidi kuhusu Jijenge , au huduma/bidhdha yoyote ya Benki au ushauri tafadhari wasiliana nasi kupitia Matawi yetu.


crdb
 
Hebu waambie vizuri, ukikopa milion 100 unalipa milion mia nne na ngapi? Kwa miaka 20?

Au hata milion 30 unalipa milion ngapi? Na malipo ya mwezi ni kiasi gani?

Frankly speaking si walimu au wenye magenge wanaoweza kopa na jijenge product. Unless mmepunguza riba.
 
ngoja tufuatilie tuone applicability yake, kama kweli na kina sisi tutapata.
 

Mbona husemi riba baada ya kukopeshwa unataka watu waingie tu kichwa kichwa then baadae ndiyo useme eti masharti kuzingatiwa
 
Siku zote watu wa benki hutoa matanagazo mazuri kweli lakini ukiingia utachoka mwenyewe sitaki mie.
 

naona hiyo ni jibomoe sio jijenge.
 
Nimeipenda hii

kajaribu uone ilivyo vigumu kudeal na CRDB katika issues za loan...usiamini wanachokisema. CRDB ni benki ngumu sana kupata mkopo tofauti na benki zingine
 

CRDB ikopeshe mtu hivi hivi??!!!...thubutu. tangu lini? CRDB ni benki ya kufanyia transactions tu.....mna maneno mazuri ya kuwahadaa share holders tu.
 
hili wazo ni zuri sana lakini kwa wachache tu..
 
Hawa jamaa ni noma,hakuna cha mkopo wala nn!masharti yao ni magumu sana.Hawana lolote.
 
unakuwa mtumwa wa bank kwa miaka 20!!
mikopo mzuri ila usiombe ukwame...
mfano unalipa mkopo miaka 15 baada ya hapo njia za kulipa zinafunga....what next??
 
Mbona husemi riba baada ya kukopeshwa unataka watu waingie tu kichwa kichwa then baadae ndiyo useme eti masharti kuzingatiwa

Hii ni business strategy ya financial institution. Utawasikia wakikuambia interest yetu ni competitive!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…