Fursa haionekani kwa Macho bali kwa akili

Mzee wa kusawazisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
1,601
Reaction score
1,172
Wakuu Leo nimeona nije na Mada hii ili ndugu zangu mlioko mjini mnufaike kupitia mawazo yangu!

Iko hivi mjini Kuna watu wengi tofauti na kijijni. Yaani Unakuta nyumba 1 Ina watu zaidi ya 20 wakiwemo wapangaji including watoto.

Kuna biashara ya vitafunwa yani maandazi ama chapati ama keki nk. Leo nije na maandazi.. Ukitengeneza maandazi 500. @1.Tsh 100 zidisha Mara 500 unapata 50000

Hapo ukitoa garama za Mafuta, mkaa ama kuni, Nguvu nk. Unakuta faida 20000 kwa siku. Zidisha siku 10 una laki mbili pembeni ya mtaji iko pale pale.

Swali unawezaje kuuza maandazi Mia 5 kwa siku?

Jibu: ukipita nyumba 1 yenye wapangaji let say 7.. Kila mtu akanunua maandazi 5 tayari 35 ukizunguka nyumba 20 tayari umemaliza kazi tena asubuhi asubui hapo hujauza wale wa njiani.

Kwa Leo naona niishie hapo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapo wamama wanapita huku mtaani wanauzaga maandazi. Lakini, kila siku watu wanakula maandazi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hizi ndio biashara za kwenye makaratasi ukifanya biashara yenyewe halisi matokeo utayaona tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo Ni Zuri! Lakini Liko Over rated, Ila Ukiwa Nje Utaona Simple, Katika Biashara Wazo Linalo Fanikiwa Ni Lile Utakalo Buni Mwenyewe Sio La Kuelekezwa, Ngumu Kuamini Lakini Ndio Ukweli,
 
Jamani sisi tunaokaa uswazi tuwe wakweli ili mwisho wa siku ukaja na maandazi yako yakakudodea, kwa taarifa yako uswazi tunapendelea sana mihogo ya kukaanga! Kwanza kwa urahisi wa bei kwa kipande kimoja, pili inashibisha tofauti na maandazi, tatu ukimix na dikodiko la mikachumbali hapo Hata mchana unaweza piga neutral.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maandazi 500 hicho ni kiwanda sasa....hapa Mwananyamala Pamechangamka hivi lakini kina mama wanalaza maandazi yao ya kwenye vibobo vya kg 8 sembuse uko kijijini wanapoamkia viporo na ndizi za kuchoma andazi linanunuliwa lipelekwe kwa mgonjwa aliyelazwa utamaliza 500 baada ya Mwaka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…