SOKO LA UHAKIKA LA VIAZI LISHE, CHANGAMKIA UPESI, LISIKUPITE!
Katika kuwajali wakulima wetu na kutambua mahangaiko yao kwenye masoko ya mazao wanayoyazalisha, kampuni ya kinasoru East Africa Tanzania Ltd imepata soko la uhakika la kuuza viazi lishe nje ya nchi kupitia wakala wao aliyepo hapa nchini. Wakati naitambulisha kwa mara ya kwanza fursa hii mpya katika mada yangu ya “Fursa Katika Kilimo cha Viazi Lishe, Tuchangamkieni Upesi”, watu wengi walikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kwa undani juu ya kilimo hiki lakini vilevile walitilia shaka uwepo wa soko la uhakika la kuuzia aina hii ya viazi.
Kwa upande wangu, nilijitahidi sana kuwatoa shaka juu ya tatizo la soko na kuwahakikishia kuwa soko la viazi lishe lipo na tena ni la uhakika, kuanzi mbegu zenyewe zile za F1 na hata viazi vyake. Nilifafanua zaidi kwa kuwaambia kuwa viazi lishe licha ya faida nyingine nyingi zinazotoa, ni chakula kitamu na chenye kupendwa sana. Na pili mwonekano wa viazi hivyo umekuwa kivutio kikubwa kwa watu wengi na kufanya visiwe na upinzani sokoni.
Mathalani, ukivuna leo tani moja ya viazi lishe vyako na ukavipeleka sokoni Jijini Dodoma kwenye soko la Maisha Plus, soko la uuzaji wa Matunda, Mbogamboga, Samaki, Ndizi na Mazao mengine jamii ya mizizi, na ikatokea kule sokoni kuna wakulima wengine wamekutangulia wenye viazi vitamu vya kawaida, pamoja na kwamba wote mna viazi vitamu, lakini wewe mwenye viazi lishe utauza mapema zaidi na kuwaacha wakulima wenzako waliyokutangulia.
Kimsingi Viazi lishe ni chakula kizuri, kitamu na chenye Vitamin A kwa wingi ambayo ni muhimu sana kwa akinamama wajawazito, wanaonyonyesha, watoto na wazee katika kusaidia uonaji wa macho, uimarishaji wa kinga ya mwili, ukuaji na kufanya maendeleo bora ya mtoto.
Watu wengi wamekuwa wakiutumia unga wa viazi lishe kama moja ya malighafi au viwambajengwa kwa ajili ya kutengenezea unga lishe wenye virutubisho mbalimbali muhimu kwa ajili ya matumizi ya makundi tofauti tofauti ya watu kama ilivyoanisha hapo juu.
Umaarufu wa unga wa viazi lishe siku za hivi karibuni umeongezeka maradufu katika jamii yetu na kusababisha watu wenye maduka makubwa kama supermarket kuutafuta unga huo kwa udi na uvumba ili kuuza kwenye maduka yao. Ndiyo maana sasa hivi siyo ajabu tena kukuta unga huu ukiuzwa kwenye aina hiyo ya maduka. Umuhimu wa viazi lishe unaoneka zaidi kutokana na kuwa na matumizi mengi.
Unga wa viazi lishe unaweza kuutumia kama ambavyo unautumia unga wa ngano kwa ajili ya mapishi mbalimbali. Unaweza kutumia unga wa viazi lishe kwa kupikia keki, maandazi, ugali, chapati na Biskuti. Aidha, viazi vyake unaweza kutumia kwa ajili ya kutengenezea Krips, Chips ama kuchemshwa kawaida au kukaangwa na kuliwa kama vitafunwa asubuhi wakati wa kupata stafutahi.
Kwa jinsi viazi hivi vilivyo na matumizi mapana, hatunabudi kukiinua zaidi kilimo hiki ili kiwe dira na mkombozi kwa mkulima katika kuinua kipato chake binafsi, kaya na taifa kwa ujumla. Kupitia viazi lishe maisha ya mkulima yanaweza kuboreka sana.
Katika jitihada zetu za muda mefu, Kinasoru East Africa Tanzania Ltd, imefanikiwa kupata soko la uhakika la kuuzia viazi lishe. Soko hilo linahitaji tani 300 sawa kilo 300,000 kwa mwezi. Soko tulilopata ni soko endelevu na ni kubwa. Mkulima mmoja au kikundi cha wakulima wachache hawawezi kumudu kutoa kiasi cha viazi kinachotakiwa.
Kwahiyo, tunahitaji wakulima wengi zaidi ambao tutaingia nao mkataba kwa ajili ya kuzalisha viazi hivyo. Na kwamba mara baada ya viazi kukomaa, mkulima atapaswa kuvipeleka viazi hivyo Dar es salaam katika ghala maalum liloandaliwa kwa ajili ya kufanya ukusanyaji wa viazi hivyo. Kama itapatikana njia nyingine bora ya kukusanya viazi hivyo kutoka kwenye mashamba ya wakulima moja kwa moja ili kurahisisha usafirishaji, basi wakati utakapofika tutawajulisha njia hiyo.
Kwa kuzingatia mzigo mkubwa unahitajika, kinasoru East Africa Tanzania Ltd, imeshindwa kuingia mkataba wa jumla na mteja wetu anaohitaji viazi hivyo kutokana na kampuni yetu kushindwa kumudu kuzalisha kiasi cha viazi kinachohitajika. Lakini hata hivyo, hadi sasa bado hatuna wakulima wa uhakika tunaowafahamu wanajishughulisha na uzalishaji wa zao hilo na wenye uwezo wa kutoa tani 300 kwa mwezi.
Ikiwa ndivyo, tukaona si vyema tukaingia tamaa kwa kujifanya tunamudu kuzalisha viazi hivyo ilihali uwezo wetu ni mdogo, ndio maana tukaamua, kwa makusudi kabisa, fursa hii muhimu tuilete kwenu wakulima wenye utayari wa kufanya kazi hii ili tuweze kunufaika kwa pamoja kupitia soko hili muhimu.
Kwa upande wetu sisi kama Kinasoru East Africa Tanzania Ltd, tutabaki kwenye kusambaza mbegu bora za F1 zenye kumhakikishia mkulima mavuno mengi kwa ekari lakini vilevile tutahakikisha kuwa kila mkulima ambaye ataingia katika programu yetu hii anapata usaidizi wa kutosha wa kiufundi katika uendeshaji wa mradi wake wa kilimo ili kuhakikisha kuwa viazi vinavyozalishwa vinakidhi ubora unaotakiwa katika soko.
Mkulima anayehitaji kujiunga katika programu hii, atapaswa kulipia ada kwenye kampuni yetu ya Kinasoru East Africa Tanzania Ltd, kwa ajili ya kugharamia ushauri wa kiufundi pamoja na kuunganishwa kwenye soko. Ushauri wa kiufundi unalenga kuhakikisha kuwa mkulima wetu anazalisha viazi bora vyenye kukidhi viwango kwa soko la kimataifa.
Aina viazi lishe vinavyohitajika kwa sasa katika soko tulilonalo ni Kabode, Mataya, Ijumla na Jewery. Na kwa bahati nzuri sana mbegu zote hizi tunazo shambani kwa hivyo ni jukumu lako sasa wewe mkulima kuhakikisha kuwa unapata moja kati ya mbegu hizo ili uendane na mahitaji ya soko.
Aidha, kama wewe ni mkulima wa siku nyingi wa viazi lishe na katika miezi mitatu uliyopita uliweza kupanda aina moja wapo kati ya aina nilizotaja hapo juu na kwamba viazi vyako kwa sasa vimekomaa na viko tayari kwenda sokoni lakini kwa bahati mbaya sana, huna soko na una ekari kuanzia mbili na kuendelea, tafadhali usikae kimya, wasiliana nasi haraka ili tuweze kuunganisha kwenye soko letu.
Bei ya jumla ya kununulia viazi vilivyokomaa ni tsh 800 kwa kilo moja na kwa gunia lenye ujazo wa kilo 100 litachukuliwa kwa tsh elfu 80. Katika mradi huu mkulima hatakopwa. Mzigo utakapofikishwa katika kituo kikuu kilichoandaliwa cha ukusanyaji, utakaguliwa kuona kama uko sawa kiubora, utapimwa uzito wake na mwisho mkulima ataweza kulipwa kadiri ya kilo alizoleta.
Tunafahamu kuwa kuna maeneo ya nchi yetu kwasasa bado kuna mvua za masika zinaendelea kunyesha lakini kuna maeneo mengine mvua hizo zimeishia. Kwa watu wanaoishi katika maeneo ambayo bado mvua za masika zinaendelea kunyesha na kuna wale ambao wako katika maeneo ambayo mvua za masika zimeishia lakini wanamudu kuendesha kilimo kwa njia ya umwagiliaji, na wangependa kuingia katika programu hii, milango iko wazi. Kila mtu anakaribishwa kuweza kushiriki katika mradi huu wenye manufaa makubwa.
Kinasoru East Africa Tanzania Ltd inatamani kuona mkulima akinufaika kupitia kilimo chake. Kama utahitaji maelezo zaidi ya ufafanuzi tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupita anuani zetu hapo chini. Hima hima wakulima! Twende pamoja, twende shambani tukalime.
Aman Ng’oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
New office location: Msalato Bible
Te: +255767989713, +255715989713 & +255786989713
Email:
amanngoma@gmail.com
Facebook Page: Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
DODOMA, TANZANIA.