Fursa: Kutengeneza vitu vya asili kwa ajili ya kuwauzia wageni (watalii)

Fursa: Kutengeneza vitu vya asili kwa ajili ya kuwauzia wageni (watalii)

Queen Rover

Member
Joined
Apr 29, 2015
Posts
88
Reaction score
79
Habari wanaJFwenzangu,

Nimepata wazo ambalo nina imani tunaweza kulifanyia kazi tukiwa kama team wawili au watatu na kuendelea. Tanzania yetu (hapa naiongelea Dar es Salaam), wageni wanaotoka nchi za nje wanaingia kila siku.

Nasema hivi kwa kuwa ni mzoefu kuzunguka maeneo tofauti tofauti kama beach na kambi ambazo hawa watu hufikia. Kiukweli wanavutiwa sana na vitu vyenye uasili wa Kitanzania na lengo langu ni hili hapa.

Unatengeneza vitu kama mikoba, pochi, viatu, bangili na vitu vingine vya kuvutia ambavyo vinaonyesha utamaduni wetu.

Tafadhali nitafute tufanye biashara wote. Tuungane tujitengenezee mabadiliko wenyewe. Camp zipo kibao wanazofikia hasa maeneo ya Beach Kigamboni.

Nitafute Whatsapp tuongee vizuri: +255 719 383 663

Karibu..
 
unao utalaamu wa kutengeneza viatu vya kitenge vya asili?
 
Back
Top Bottom