The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Umoja wa Ulaya (European Union) wametoa wito kwa ajili ya kuwasilisha maandiko ya miradi (Concept Notes) kwa Asasi za Kirai nchini Tanzania. Lengo mama (Overall Objective ) la E.U katika wito huu (Call for Proposals) ni kuimarisha Asasi za Kirai na watetezi wa haki za binadamu katika juhudi zao za kupigania haki za binadamu, uhuru na demokrasia.
Lengo hili linaendana na AGENDA 2030 pamoja na Malengo Endelevu ya Maendeleo (Sustainable Development Goals).
Jumla ya kiasi kilichotengwa kwa Asasi za Kiraia katika utekelezaji wa Miradi ni zaidi ya Shilingi za Tanzania 6,000,000,000.
Kiasi cha chini kuombwa kinapaswa kuwa Shilingi 1,171,116,000 na kiasi cha juu kuombwa kinapswa kuwa shilingi 2,342,232,000.
Ili mradi ukubaliwe (being accepted), unapaswa utekelezwe sehemu yoyote nchini Tanzania, na muda wa utekelezaji unapaswa kuwa kati ya miaka miwili (2) mpaka mitatu (3)
Nani anastahili kuomba fedha hizi?
- Asasi za Kiraia (Civil Society Organizations)
- Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs)
- Taasisi za Kisheria (Legal Entities)
- Mashirika ya Kijamii (Community Based Organizations)
- Mitandao (Networks)
- Kuhakikisha ushiriki wa vijana na wanawake katika masuala ya habari (media)
- Kuchochea uhuru wa kujieleza na upatikananaji wa habari kwa wananchi wote
- Kuzijengea uwezo Asasi za Kirai na wadau katika tasnia ya habari katika uwasilishaji na , ufuatailiaji juu ya masuala yahusuyu uhuru (fundamental freedoms)
- Kuchochea ushiriki wa mtu mmoja mmoja na na jamii kwa ujumla kwenye usuluhishi wa migogoro.
Mwisho wa kutuma Maombi ni tarehe 07/05/2019
Ahsante
The Consult; +255 719 518 367
E-mail ; theconsult38@gmail.com
Dar es Salaam
Tanzania
Home of Project Management, Strategic Management & Fundraising Strategy