Fursa mbalimbali katika Sekta ya Bahari zenye kuingiza kipato kikubwa

mkuu hv fursa namba 2,4,6 zinahitaji minimum capital kias gan mana nmekuta narudia rudia sana kusoma huu uzi
Mtaji inategemea unataka uwe unahudumia meli zipi kama utafanya Ship Chandling. Meli kubwa za mizigo kama za ngano wanakaa muda mrefu baharini usishangae wanakupa oda ya ngombe 2 mpaka 4.

Kama ukianza hata na mtaji wa 1 million unaweza ukafanya biashara na
mtaji mdogo ukawa unachukua bidhaa kwa mali kauli kisha ukilipwa unalipa pesa ya hizo bidhaa.

Hiyo ya kutoa mafuta ukifungua mtaji itakuwa ni gharama za kuwalipa vibarua na kukodi gari.
 
Safi kbs. Ntarudi kucheki tena
 
ok
 
Kama hii ya kutoa taka taka melini si kila mwaka si mnaomba tenda au ukisha jisajili ni basi
 
Mkuu sasa kama natoa mafuta machafu kwenye meli naenda kuyamwaga wapi maana serikali kila sehemu wanasema unaharibu mazingira je hayo mafuta machafu yanaweza kutumika kwa matumizi gani mengine kwa mtaji wangu wa milioni 3 si utanifaa kukodi nyonya mafuta
 
Hapo safi sana brother hivi mabaharia kutokana na kukaa sana baharini nilikuwa sijui kama wanahitaji chakula sana nilijua wanakula fast food na juisi sana
 
Dah mkuu samahani hii diesel chafu wanaenda kufanyia nini
 
Mkuu mbona niliulizia bandarini nikaambiwa na chanzo ninachokiamini Cha taarifa kuwa hizo huduma zote zinatolewa na Serikali kupitia shirika lao flani nimelisahau jina lake..


Kwa jinsi alivyoniambia sio rahisi kufanya haya uliyoandika pale bandarini kwa mtu binafsi.
 
Ni shughuli zipi ulizo uliza mkuu.
Tasac inafanya usimamizi kwenye masuala ya uwakala wa meli na usimamizi wa utoaji mizigo.

Utoaji mafuta machafu, kusupply vyakula melini hizi kampuni ni za watu binafsi.
Maeneo ya Mivinjeni kuna kampuni moja ya Ship Chandler na kuna jamaa yangu Boss wake ana kampuni ofisi nyumbani wana supply mahitaji melini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…