Fursa mpya kwa mwaka 2018

Fursa mpya kwa mwaka 2018

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Heri ya sikukuu wadau,
Kwa kuwa mwaka unaisha na kwa kuwa naamini katika kutengeneza fursa naona ni washirikishe moja ya mipango yangu kwa mwaka 2018 tushauriane.

Kwanza kibasa mfahamu hili swala nimelifanyia utafiti wa kina na bado utafiti unaendelea kwa hiyo yeyote ambaye anaona fursa na angependa kuweka pesa yake hapa basi anaweza kutoa mchango wake.

Nchi yetu ni nchi ya Uchumi wa viwonder ila ninataka tushiriki katika kuifanya kuwa nchi ya Viwanda.Kwa kuzingatia hilo nimepanga kufanya lifuatalo.

Ninampango wa kuanzisha kampuni itakayohusika na Network Marketing au biashara ya Mtandao ambayo italenga kuuza bidhaa na huduma za kitanzania tu.Kwa lugha nyingine tutakuwa tunauza huduma na bidhaa zinazotolewa na watanzania ndani ya Tanzania.Bidhaa hizo na huduma hizo ni pamoja na bidhaa zinazozalishwa na wafanya biashara ndogo ndogo in small scale.Hasa wale wanaoshirikiana ama na VETA au SIDO pamoja na taasisi zingine

Kampuni itakuwa na malengo makuu mawili kuweka mfumo mzuri wa Quality Control kwa bidhaa na huduma zote zinazozalishwa hapa Tanzania na Pili kufanya Branding na Promotion ya Bidhaa zinazozalishwa hapa Tanzania.

Malengo haya yatafikiwa kwa kutoa mafunzo na kuwaunganisha wajasiriamali na masoko ya mitaji na kuwaunganisha wajasiriamali na wateja.

Katika mfumo wetu kutakuwa na aina tatu ya wanachama.Wanachama Wawekezaji,Wanachama Watumiaji na Wanachama wazalishaji

Gharama za kujiunga katika mfumo huo zitalingana ingawa huduma mtu atakazopata zitakuwa tofauti na mtu anaweza kujiunga katika makundi yote matatu.

Unapojiunga kama muwekezaji utapewa fursa ya kukutana na wazalishaji wanaohitaji mitaji kuzungumza nao na kuangalia jinsi ambavyo unaweza kuwekeza kwao.

Unapojiunga kama mzalishaji utakutana na wawekezaji ambao watawekeza katika biashara yako na utakutana na wateja watakaonunua biashara yako

Unapojiunga kama mteja utapata fursa ya kununua bidhaa kwa matumizi yako au kwa ajili ya kuziuza kwa wengine.

Pamoja na faida tajwa hapo juu.Kila utakapoalika watu wajiunge kama wawekezaji,wazalishaji au watumiaji utapata kitu kinaitwa profit share value(PSV) ambayo itakuwezesha kuwa mwanahisa katika kampuni mama.PSV itakuwezesha kupata gawio kila mwezi kulingana na faida inayopatikana katika uzalishaji na mauzo.Thamni ya PSV itapanda na kushuka kulingana na mapato matumizi na faida.

Kadiri unavyounga watu wengi ndivyo PSV yako inapoongezeka kwani mtu mmoja ni sawa na PSV moja

PSV haziuzwi na zinabaki kuwa mali ya mwanachama.

Ukokotoaji wa PSV hufanywa kwa downlines business volume yaani faida ni kutoka na total sales za waliojiunga chini yako.mpaka kizazi cha nne ambapo kizazi cha kwanza ni 1 PSV cha pili ni 0.1 PSV cha tatu ni 0.01 PSV na cha nne ni 0.001 PSV kwa hiyo tunapokokotoa PSV TUNAJUMLIMSHA PSV MPAKA KIZAZI CHA NNE.

KUNA KIWANGO CHA PSV UKIFIKA UNAPANDA DARAJA


Unapokuwa mwananchama katika makundi yote unaweza tengeneza faida kwa njia nyingine za ziada kama vile kuwekeza kwa mfanya biashara ambapo unapowekeza kwake unakuwa unapata taarifa za biashara yake na hivyo anapopata faida unapata gawiwo la faida kulingana na uwekezaji wake kwako.Unapokuwa mteja una uwezo wa kuchukua bidhaa na kuziuza kwa rejaraja na kupata faida ya commision ambayo ni ya kwako.Unapokuwa mzalishaji unaweza kuuza bidhaa zako ama in system au outside the system na kuendelea kutengeneza faida.


Wazo hili bado liko kwenye hatua ya utafiti na development.


Tunahitaji web system inyoweza kusimamia mfumo wetu kama tulivyoeleza,tunahitaji wazalishaji wa bidhaa ambao wana uzoefu wa uzalishaji

Mpango ni kushirikiana na SIDO na VETA TBS,TFD TCCIA ili tuweze kutengeneza wazo zuri na lenye TIJA kwenye wazo hili


Povu,Wenge maswali na maoni,nakadhalika vinakubalika kabisa
 
a very good idea!
will you have a specific area to conduct these activities or will it be an online system based activity..!!?

Network marketing ni nzuri navutiwa nayo ila bado sijaijua vizuri na hata wengi pia hawaifahamu so nashauri ukianza kuImprment your idea usisahau na elimu kwanza kwa wananchi ili utushawishi kuungana na ww kutumia hii fursa.

All in All thank you for sharing, thats very kind of you.
 
Thanks for asking,
It will be both:We will have zonal offices in Kilimanjaro,Dar es Salaam Mwanza and Mbeya with and else where.At the moment we are only in Moshi but not yet operational we are still pulling together resources both financial and human,but the online system will be at the core of the business.

We will have a quality management system in which we will work closely with SIDO and VETA TBS TFDA and TCCIA as we believe they will have a role to play.

There will be a training and we are actually working to develop a curricula to teach Network Marketing as we believe that it will speed up the growth of small scale producers.
 
Thanks for asking,
It will be both:We will have zonal offices in Kilimanjaro,Dar es Salaam Mwanza and Mbeya with and else where.At the moment we are only in Moshi but not yet operational we are still pulling together resources both financial and human,but the online system will be at the core of the business.

We will have a quality management system in which we will work closely with SIDO and VETA TBS TFDA and TCCIA as we believe they will have a role to play.

There will be a training and we are actually working to develop a curricula to teach Network Marketing as we believe that it will speed up the growth of small scale producers.
well, i will look forward to learn and hear more about this.....i hope it will bring positive impact to our societies there, most especially to teenagers.
 
Back
Top Bottom