Fursa muhimu ya kujifunza ujasiriamali toka kwa wajasiriamali wasomi wa SUA walioenda Uturuki

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
2,973
Reaction score
3,904
WanaJF,
Majuzi nilikuwa nawasikiliza wasomi wa SUA walioenda Uturuki na kurudi na taaluma nzuri hoticulture. Ktk maelezo yao nilifurahi JInsi ambavyo unaweza kulima hekta moja (eka 2 na nusu) na kupata faida kubwa sana ndani ya mwaka mmoja. Gharama ya semina hiyo ya siku moja ni Tsh 65,000. Itafanyika tarehe 11kuanzia saa mbili asubuhi, ktk ukombi koma koma house mwananyamala, mkabala na jengo la Bank ya Akiba Commercial Bank. Kwa maelezo zaidi kuhusu Location mpigie mkurugenzi wao (0617 135869)

NB. Mimi siyo sehemu ya hiyo kampuni ila natoa fursa kwenu ninyi wanajf ili tukafaidi wote.
 
Mkuu ungedadavua japo kidogo ni kipi walichozungumza kuhusu hilo walilojifunza huko Uturuki, kuna members humu wapo nje ya Dar hawataweza kuhudhuria hio semina
After all kwanini wanachaji kiasi kikubwa hivo, kama wao huko Uturuki walipelekwa kwa gharama za Serikali au mfadhili yoyote kwanini wao nao wasitoe hio Elimu bure kwa faida ya watanzania woote
 
Badala wakalime ili wapate wao hiyo faida wanayoizungumzia wanataka kula pesa yetu. Practical hawataki kuapply, wao theory tu!!
 
Mimi sijaweza kueleza kila kitu.Hawa jamaa wanazungumza kupata faida ya zaidi mil 100 kutoka kwenye hekta 1 (eka 2 na nusu) Ni teknolojia mpya nzuri sana. Nimeridhika na maelezo yao ndo maana nikawashirikisha. Ktk pesa hizo 50,000 inaisha kwenye chakula na ukumbi tu. Hakuna faida kubwa hapo. Hilo swali aliulizwa na Mwanndishi na akajibu hivyo.
 
Nashauri kwa mjasiria mali wa kweli hii siyo semina ya kukosa. Kwamba kwanini wao wasiende porini kulima siyo hoja. Wao wanalima na wanatufundisha. Wakiacha kutufundisha tungepata wapi taaluma hii??
 
Mimi sijaweza kueleza kila kitu.Hawa jamaa wanazungumza kupata faida ya zaidi mil 100 kutoka kwenye hekta 1 (eka 2 na nusu) Ni teknolojia mpya nzuri sana. Nimeridhika na maelezo yao ndo maana nikawashirikisha. Ktk pesa hizo 50,000 inaisha kwenye chakula na ukumbi tu. Hakuna faida kubwa hapo. Hilo swali aliulizwa na Mwanndishi na akajibu hivyo.
Ni zao gani specifically la bustani wanazungumzia? au ni yote
 
Mimi sijaweza kueleza kila kitu.Hawa jamaa wanazungumza kupata faida ya zaidi mil 100 kutoka kwenye hekta 1 (eka 2 na nusu) Ni teknolojia mpya nzuri sana. Nimeridhika na maelezo yao ndo maana nikawashirikisha. Ktk pesa hizo 50,000 inaisha kwenye chakula na ukumbi tu. Hakuna faida kubwa hapo. Hilo swali aliulizwa na Mwanndishi na akajibu hivyo.

Sawa Bwana Aweda. Kupata faida ya 100 Mil kwenye Hekta Moja inanipa mashaka kama hawa watu wako Siriaz, labda kama umewa-mis quote.
 
Napenda practical, sio porojo za theory, isijekuwa hyo semina wanayotoa ndio ujasiriamali wao, lol! Tunataka experience zao ktoka field
 
WanaJF,
Majuzi nilikuwa nawasikiliza wasomi wa SUA walioenda Uturuki na kurudi na taaluma nzuri hoticulture. Ktk maelezo yao nilifurahi JInsi ambavyo unaweza kulima hekta moja (eka 2 na nusu) na kupata faida kubwa sana ndani ya mwaka mmoja. Gharama ya semina hiyo ya siku moja ni Tsh 65,000. Itafanyika tarehe 11kuanzia saa mbili asubuhi, ktk ukombi koma koma house mwananyamala, mkabala na jengo la Bank ya Akiba Commercial Bank. Kwa maelezo zaidi kuhusu Location mpigie mkurugenzi wao (0617 135869)

NB. Mimi siyo sehemu ya hiyo kampuni ila natoa fursa kwenu ninyi wanajf ili tukafaidi wote.

-thought of the opportunity... mouth watering
- Reality of the opportunity... mmmhhh.. a demo is needed here.
-Venue location and conference package (not their fee)... I am uncomfortable!! there are standard hotel facilities at an affordable rates.. hata kule tunapopata kikombe cha chai... si kila anaekwenda pale lazima ale mlo wa hoteli...!!
 
WanaJF,
Majuzi nilikuwa nawasikiliza wasomi wa SUA walioenda Uturuki na kurudi na taaluma nzuri hoticulture. Ktk maelezo yao nilifurahi JInsi ambavyo unaweza kulima hekta moja (eka 2 na nusu) na kupata faida kubwa sana ndani ya mwaka mmoja. Gharama ya semina hiyo ya siku moja ni Tsh 65,000. Itafanyika tarehe 11kuanzia saa mbili asubuhi, ktk ukombi koma koma house mwananyamala, mkabala na jengo la Bank ya Akiba Commercial Bank. Kwa maelezo zaidi kuhusu Location mpigie mkurugenzi wao (0617 135869)

NB. Mimi siyo sehemu ya hiyo kampuni ila natoa fursa kwenu ninyi wanajf ili tukafaidi wote.

Thank you Bw. Aweda kwa utambulisho huu na pole kwa comments. namba yangu ni 0717 135 869. Nimefurahia sana mjadala. Kwa ukweli Tanzania hatufanyi vizuri sana kwenye soko huru la pamoja la dunia (free common market), yaani tunaletewa zaidi kuliko sisi kupeleka nje ya nchi. hata tunavyopeleka hatuviongezei thamani (unajua km kilo moja ya pamba hutoa mashati 3! sasa kwanini tupeleke pamba badala ya mashati, kwanini tupeleke maembe badala ya juice. Hivyo tumekuwa taifa la wachuuzi na watumiaji. Kilimo chetu kimekuwa cha kujikimu na ile dhana ya kilimo ni uti wa mgongo hidhiiriki sana.
Ndugu zangu hapa hakuna wa kumlaumu. Agriculture Media tumeona tatizo kubwa ni mtazamo kwa watanzania. Kutokujiamini, vipaombele na ujasiri katika shughuli za kiuchumi.
Kampuni imeona sehemu pa kuanzia ni matumizi bora ya taarifa na teknolojia katika kilimo ndipo patakapo tutoa. Hivyo tumeanzisha program ya Kilimo cha kibiashara na ufugaji wa kibiashara. tutumie ardhi kidogo mazao mengi, mifugo kidogo mazao ya mifugo mengi kisha tuongeze thamani ya mazao yetu ili tukauze nje ya nchi yetu hapo ndipo kilimo kitachangia kwenye GDP na uchumi wa nchi yetu utakuwa kwa kasi. Lakini tukitegeme utalii, usafirishaji, mawasiliano hatuwezi kutoka hapa tulipo. Nawatakia siku njema wakuu
 
. Agriculture Media tumeona tatizo kubwa ni mtazamo kwa watanzania. Kutokujiamini, vipaombele na ujasiri katika shughuli za kiuchumi.

Agriculture Media..Start ups?Office Location Sir? web/blog? portfolio?!.. ni udadisi tu....
 
Hivi ni lazima semina muhimu kama hiyo ifanyikie sehemu za gharama kama hotels,kwanin wasitumie hata kumbi za shule siku za weekend watanzania wengi wakapata fursa?
 
Badala wakalime ili wapate wao hiyo faida wanayoizungumzia wanataka kula pesa yetu. Practical hawataki kuapply, wao theory tu!!

Mkuu Barraza nawe ulishawashitukia eenh! Nawakubali madaktari wa binadamu hufundisha na unawakuta vyumba vya upasuaji, na wanafungua zahanati na hospitali lakini wajanja wa sekta ya kilimo mwee kilimo cha mdomoni na kwenye karatasi.
 
Siku moja nilikwenda SUA 2011 pale chuoni, nikakuta kidimbwi chao cha kufugia samaki kimekauka, jamaa ndio wakasema nenda Kinguluira utapata darasa. Hao jamaa pamoja na kufundisha wawe na mashamba/bustani ili sisi tukaone kwa macho ya nyama, macho ya rohoni kwenye kilimo not applicable.

Mimi wakinionyesha sehemu wanayotolea/download ujuzi wao nitaenda kuwasikiliza. Angalia wabongo tulivyo, Bwana shamba, yy shamba hana, Bwana nyuki, hata mzinga mmoja hana, Bwana samaki, hata kidimbwi hana.
 
Hii nchi yetu n vigumu sana kuendelea Jamaa kama hao baada tu ya kupata elimu ilitakiwa sasa hivi wawe wako Chaka na wanapiga jembe vibaya, sasa chakusikitisha ni kwamba hawa jamaa utakuta wanatafuta kazi huko Dar na wamona waanze na Tuition za bustani kwanza, Na unaweza kujiuliza walienda vipi huko kama walikuwa hawana nia ya kulima? au ndo yale mambo ya kukuta Maonyesho ya Utalii huko Ulaya badala wapelekwe watalaamu wa Utalii unakuta anaenda Engenear wa Hifadhi mara Mhasibu Mkuu, mara Mkuu wa Madreva wa Hifadhi, hii nimeishuhudia,

Ni vigumu sana sisi kusonga mbele
 
Naongezea kidogo hapo hapo, hivi Dar kuna wakulima kweli? maonyesho ya nane nane hayafanyiki Dar miaka yote kwa sababu hakuna wakulima.
Semina hizi wangeleta kwetu tunaolima huku Iringa, Arusha,Moro,Katavi nk, ambako hata maafisa wa serikali wana vishamba vya kuzugia week end.

Nyie Wasomi tumieni muda huo kwa wahitaji wanaomaanisha ambao wako vijijini na mikoani. Njooni kwetu Mby tunawahitaji sana mje mtuseminishe ili tuongeze tija la kilimo cha Super Kyela !!!!!!!.
 
Mkuu waje Vijijini na Dar wamuachie nani? Ndo maana nasema ni Vigumu sana Tanzania kusonga mbele kama wataalu wa Kilimo, Ufugaji wa Nyuki, Kuku, samaki n kazalika wako Dar, Huku vijijini wananchi wenye spirit ya Ujasrimali hujikuta wanafanya bora liende n kikubwa elimu ya kuwa boost hawapati kabisa, make watalamu wako Dar mitaa ya Posta
 
Back
Top Bottom