Fursa ya biashara ndani ya visiwa vya Comoro

Mzee mwenzangu vipi!? Ulifanikiwa!?
 
Zanzibar pia ni 99% islam lakini kitimoto inauzika kama kawa.

Zanzibar kuna wabara wengi wakristo wanaishi kule, pia kuna utalii kwahiyo wazungu ni wengi sana maeneo ya mashamba.
 
Vipi ulifanikiwa kwenda Comoro?
Mimi naelekea huko hivi karibuni
 
Chakula cha aina gani? Hata matoke ya Bukoba wanayahitaji? Au ubwabwa tu?
 
Ukiwa hapa Mtwara mitaa ya Chikongola utashuhudia lundo la Wacomoro wakija kufata bidhaa Tanzania.
Kwenye mtaa huu kuanzia guest house za Chilindima kuja hadi huku inapoishia Tiffany hotel kote wanajaa hawa jamaa. Ila guest yao pendwa ni Obrigado au Chalinze maana hapo ndio wanaona ni sehemu salama kuweka vitu vyao.
Wakifika Mtwara hapa wanaanza kupanga mipango ya safari ya kuja Dar, wana jamaa yao ambaye ni Mcomoro pia lakini anaishi Dar. Huyu jamaa huwa wanamtumia katika mizunguko yao hasa wakishaingia Tanzania, wanamlipia hela anakuja Mtwara anatafuta usafiri wa kuja Dar, wakifika huko anawatembeza kununua bidhaa na kurudi nazo Mtwara.
Hawa jamaa huku Tanzania wanakuja na meli yao wakiwa wameikodi, wananunua bidhaa nyingi sana yani ni kila kitu kilichopo mbele yao wananunua.
Leo wameondoka na nimeongea nao wanapanga kurudi tena mwezi wa sita kuhemea tena.
Comoro sijafika ila kwa mizigo walonunua hawa jamaa inaonyeaha dhahiri kuwa pesa ipo kama utapata mwenyeji kule.
 
Dah.. yaan natamani sana kupata connection nao.. chukua number zahuyu jamaa yao wa Tz ili niongee naye
 
Alichoongea mtoa mada ni kweli kabisa kuhusu fursa za biashara Comoro, nakumbuka mwaka 2018 tuliungana watu kadhaa tukajichanga ili tukodi meli ya kupeleka bidhaa Comoro na biashara tuliyoikusudia ilikuwa mbuzi. Tulifanikiwa kweli kukodi hiyo meli kwa mmiliki kutoka Zanzibar kwa milioni 46.

Baada ya kukamilisha process zote za vibali mbuzi walichelewa kidogo kupatikana kutokana na idadi tuliyokusudia so ikabidi tupeleke kwanza mizigo ya wafanyabiashara wengine then meli ikirudi ndo tuanze biashara yetu ya mbuzi kama kawaida. Tulimchagua mwenzetu mmoja aende na meli na kupokea malipo yote ila baada ya kuondoka na ile meli na kupata malipo akatokomea.

Tulifuatilia sana hadi kwenda mahamani ila ndo hivyo tena haikuwezekana ikabidi kila mtu ashike njia yake maana wengi walikuwa very disappointed, mpaka leo plan nzima ya biashara ipo kwenye pc yangu huwa naiangalia tu but I know oneday hii biashara nitaifanya tu sijakata tamaa.
 
Ndugu soko la mbao kule ni changamoto asikudanganye mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…