Fursa ya biashara ya uume wa ng'ombe

BrazakakaBura

Member
Joined
Feb 16, 2017
Posts
88
Reaction score
104
Heshima kwenu wakuu,

Ni muda sasa tangu nifahamu biashara hii lakini kwa bahati mbaya hakuna uzi hapa jf unaoelezea biashara hii, naamini kuwa connected ni kitu bora zaidi kwenye biashara yoyote.

Kuna wachina hapa mjini(Dar), japo kwa sasa hata mikoani wamefika, wananunua vitu vingi kutoka kwa wanyama specifically niongelee ng'ombe, ambapo wananunua uume zilizokaushwa vzuri, bei hubadilika badilika kwa sasa ni kati ya 12000/= na 16000/= kwa kilo moja, lakini pia wananunua pembe, ngozi, nyongo, kwato, vitabu(kuna vitu ndani ya ng'ombe vinaitwa vitabu), kuna wakati kabla ya corona bei ilipanda hadi kufikia zaidi ya 20000/= kwa kilo moja, kitu ambacho kinatarajiwa badae kidg utafikia huko tena,
hizo uume lazima ziwe zimekaushwa zikiwa zimenyooka vzuri inatakiwa kutoa layers flani ina mafuta mafuta then unaanika zikiwa zimenyooka.

Kuna wengine ni wazoefu mikoani unaweza kununua zilizoandaliwa vzuri ziko tayari kabisa kwa garama nafuu kutegemeana na sehemu, mfano unaweza kupata kwa 7000/= kwa kilo then ukauza kwa 14000/=

kama wapo wazoefu tubadilishane mawazo, na kuwasaidia wageni, kwa asiyejua kabisa ulizia sehem yoyote ya machinjioni.

Zaidi, soma:

1). Kwa hapa Tanzania, Wachina hununua gramu1 ya Gallstone (Nyongo) Tsh. 8000 mpaka 10000
 
Uko sahihi mkuu binafsi nilifikiri huenda imeanza recently lakini kumbe ni miaka mingi wananunua hivi vitu ambavyo hatuwezi kuzania kirahisi
Kuna jamaa yangu yuko kwenye mabasi kuna kipindi alipakia mzigo huo toka Tunduma alipomtajia bei ya mzigo jamaa alilipa bila wasiwasi alipomuuliza unaenda wapi akamwambia wachina wanachukua.
 
Niliwahi kuipiga hii business mara moja..nilinunua hizo kwa elfu 5 huko Morogoro, nikaja kuziuza kwa elfu 13,000/= @ kwa wachina flan walikuwa vingunguti baada ya covid 19 kuingia wale wachina walienda kwao na hawajarudi mpaka leo..

Niliwahi kuwahoji wanazifanyia nini hizo dudu za ng'ombe wakajibu zinatumika katika kutengeneza vifaa vya hospitalin ingawa hawakuniambia ni vifaa gan.
 
Kwa kilo 1 elf 13 au kwa kila uume elfu 13
Maana mdau upo kazungumzia biashara inafanyika kwa kilo moja
Labda kwa uzoefu uume unakuwa na uzito gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…