Fursa ya kuuza mahindi Congo

Fursa ya kuuza mahindi Congo

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
2,968
Reaction score
8,139
Wadau, chekini taarifa ya fursa hiyo hapo chini kutoka TCCIA;

Ndugu Viongozi wa TCCIA,

Tunapenda kuwajulisha kuwa tumepokea barua kutoka Wizara ya Viwanda,Biashara na uwekezaji kwamba Ofisi ya RAS-Songwe kwa kushirikiana na TCCIA walifanyia kazi fursa ya kuuza mazao ya chakula huko DRC kwa upendeleo maalum na kufanikiwa.

Kufikia makubaliano na Uongozi wa Jimbo la Haut-Katanga umetoa Kibali cha miezi minne(4) kuanzia tarehe 1 Desemba,2018 hadi Machi31,2019 kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuuza chakula katika jimbo hilo kwa kiwango chochote walichonacho pasipo kulipa ushuru.

Makubaliano hayo yameeleza kuwa,baada ya kipindi hicho hawataruhusiwa kuuza kwa utaratibu wa kawaida ikiwa ni pamoja na kulipa ushuru.

Hivyo kwa makubaliano hayo,Tani moja(1) ya mahindi itauzwa kwa USD350,Unga wa Mahindi USD 400,Maharage na Mchele USD1,120.Bei hizi ni pamoja na gharama za uchukuzi.

Hivyo wafanyabiashara wote mnashauriwa kutumia fursa hii.

Asanteni sana kwa ushirikiano.

For more enquiries

hq@tccia.com

TCCIA
 
Rekebisha hapo kwenye
Tani 1 ni USD 350
Nadhani ni
Kilogram 1 ni USD 350
 
Nahisi sasa wameanza kumwelewa Jiwe. Magu anataka mambo kama haya
Yap
Ni kweli mkuu.

Na ninadhani soon aliyeleta wazo hili na kulifanyia kazi anaweza kuwa promoted kuwa motivate na wengine waige mfano
 
Huko kwenye vita, ndo biashara ya chakula inalipa zaidi mkuu Isanga family
Mkuu kuna jamaa etu mmoja alienda Sudan kusin na pick up alitoka nalo SA kaenda kariakoo kanunua nguo na vitu vingine vya kumwaga alivuta tela pia tripu ya kwanza aliuza ya pili alitoka SA kawashawishi na wengine wawili waliyaacha magari na mizigo huko walirudi na kandambili sema jamaa ni mpambanaji alikuja kufanikiwa kwa kufanya biashara Zambia...Wacongo waje wanunue wao tuwauzie kwenda kwao mgeni ni wajanja wajanja sana na matapeli..
 
Wazo mgando, usifkilie kufa kwenye utaftaji....wote tungekua na akili ka yako migodi yote isingekua na watumishi
Mkuu lazima ufikiri swala la risk pia kama kutafuta kunakufanya uhatarishe maisha yako kwa sababu ya fedha basi utakua mjinga sana,mgodi mbona ipo salama tuu
 
Back
Top Bottom