Fursa ya utengenezaji sandals Kimasai

Fursa ya utengenezaji sandals Kimasai

Gluk

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
1,859
Reaction score
3,008
Kwa utafiti niliofanya kuhusu biashara ya sandals za Kimasai kwa sasa hazina ubora, sandals unavaa muda mchache zinaanza kubanduka tofauti sana na miaka ya nyuma kuaribika kwake ni kuisha kwa sandals.

Kama wewe unaweza tengeneza hizi sandals za kimasai jaribu kuboresha na kuja kitofauti kabsa na zilizopo sokoni. Wanaofanya kwa sasa wanafanya kwa mazoea hawaangalii ushindani kwasasabu wote wanafanya sana hakuna utofauti.
Hii sasa ndo fursa yenye pesa za kutosha kama utaweza kuja na aina hiyo hiyo ya sandals lakini imara zaidi kuliko zilizopo sokoni.

Siku zote kumbuka badilisha majanga kuwa fursa, sandals zilizopo sokoni kwa sasa ni majanga mimi naongea hili kwasababu ni mvaaji mkubwa sana kama sio mdau wa sandals za Kimasai.

Fanya utafiti wa kina kuhusu ubora au angalia sandals za kimasai za Kenya linganisha na za Tanzania utaona utofauti mkubwa zaidi wa ubora.

Boresha lakini weka bei ile ile ya sokoni ila waonesha utofauti wa ubora kwa kuwaonesha kwa kurekodi video na kupost Instagram.

Waelezee kwanini sandals zako ni bora na tofauti kuliko zilizopo sokoni. Kadhani sana kuelezea kwenye utofauti usitoke hapo maana ndiyo wateja wanapotaka kusikia kuliko ubora.

Wafanyabiashara wengi wanapenda kusoma bidhaa zao ni bora lakini wanasahau kuonyesha utofauti ulipo kati ya bidhaa zao na ziliopo sokoni.

Kuna msemo mmoja unasema: "Wengi wanapenda kujiita lakini hawapendi kuwa".

Wengi wanapenda kunadi bidhaa zao ni bora lakini sio bora kama wasemavyo, hicho kitu wateja wamekichoka kukisikia kwenye masikio yako wanatka utofauti.

Ukitaka ufanikiwe kwenye biashara ya aina yoyote ile jikite kwenye utofauti jumlisha na ubora. Penda kuwaonesha wateja wako utofauti.

R.I.P Mengi
 
Gluk,

Umeongea ukweli mkuu.

Mimi mwenyewe nilinunua hizo sandals nikavaa wiki 3 zikakatika zikaniboa tu nikaachana nazo. Baada ya hapo nikaenda kariakoo nikachukua sendo za ngozi kwa Bei ya 35000 Tsh.

Najua hii ni mkataba nitavaa hadi nichoke mwenyewe.
 
Umeongea ukweli mkuu.

Mimi mwenyewe nilinunua hizo sandals nikavaa wiki 3 zikakatika zikaniboa tu nikaachana nazo. Baada ya hapo nikaenda kariakoo nikachukua sendo za ngozi kwa Bei ya 35000 Tsh.

Najua hii ni mkataba nitavaa hadi nichoke mwenyewe.
Tatizo wabongo wengi tunapenda vitu bei rahisi bila kuangalia ubora wa unachonunua.
 
Back
Top Bottom