Fursa za biashara Zanzibar

Nasikia kuna soko zuri sana la kiazi mviringo huko.
 
Mi nadhani tatizo lipo kwenye kupata habari na uwoga wa ku take risk.Wengi hatupendi kuumiza kichwa katika kuwekeza that's way tunakuwa na excuse nyingi.John Rockefeller àliwahi Judea"I always try to change Avery disester into oppunities. Kitu ambacho hatuna uwezo huo
 
Mambo mengine au ukitaka kujua fursa za kibiashara Zenji muwe mnauliza wenyeji msiende kichwa ngumu na kufanya Survey zenu pekee na kujiridhisha tu, ohoo mtakuja kupoteza mitaji yenu na kujutia baadae
 
thanks ila tunasafari ndefu
 
Vipi kuhusu lile zuio la ku-export mazao nje si utahitaji vibali na mambo ya urasimu yanajaa.
 
Ni kweli kuna fursa lakini pia kuna ubabaishaji mkubwa sana wa kuingiza mzigo kutoka bara ...sio hizi za hotel hata biashara ya mbao ngumu inalipa sana Zanzibar.... Kuna mitumbwi inapitia Bandar ya mtwara na tanga ni karibu sana but mchakato wa vibali inabidi uwe mtu wa mtaji mkubwa embu fanya reserch na wewe kujua kwann watu hawachangamkii hiyo fursa...hakuna fursa mpya hapa tz kwa biashara za namna hiyo
 
Hata bangi inalimwa hapahapa halafu watu wengine wanaingiza kutoka nje. Tatizo commitment.
 
Tumejaa ulaghai, uongo, utapeli, maneno mengi yasiyo na maana, uzinguaji, no commitment, porojo, visingizio, karaha na kila hila. Hayo yote hayatakiwi kwenye biashara ya leo.
 
Kuna tatizo pia kuhusu elimu ya jinsi ya kuanza biashara. Masoko ya mitaji, mifumo ya kodi, changamoto sokoni. Mfano: wanaotoa elimu kuhusu fursa za kilimo Hakuna anayezungumzia changamoto kubwa Kwa mkulima mwenye mtaji mdogo: source of sustainable labour(wafanyakazi WA uhakika) mifumo ya masoko yetu(changamoto za madalali na ushuru usioangalia Hali ya soko) na kadhalika. Hivyo basi na Huku watu waelimishwe. Watu wanaogopa changamoto za kuanguka kimitaji pia.
 
Tatizo kodi..yaani jinsi ya kupitisha mzigo kuupeleka mpaka zanzbr...TRA
 
Nina papai za kutosha so waliopo huko tujuzane bei Mimi nipo tanga
 
Shida kubwa bandarini unapigwa kodi km unaenda ulaya,haiwezekani unatoka zenji na friji lako au tv unafika bandarn unalipishwa wakt uko within country
 
Nauza nyama ya ngombe , huko zanzibar kuna fursa nilete nyama ,connection please wadau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…