Daktari wa Meno
JF-Expert Member
- Sep 5, 2019
- 509
- 1,610
Mimi nilipoanza kulima ndipo niliona Dar kuna vijana wazembe sana yaani wamekaa na wanawaza kuuza viatu na nguo tu hakuna mawazo mbadala yaani hawawazi mambo makubwa.
Nimetoka Dar na nimefanikiwa katika kilimo ila Dar wanawaza tu kufungua maduka ya nguo, viatu na simu. Mfano kijana hapo Dar kuna magunia mengi ya mkaa yanaingia kila siku kutoka maeneo mbalimbali ukichukua magunia yako 10 na Canter upeleke Morogoro au Tanga ndani ya siku 3 mkaa umeisha unarudi Dar kufunga mzigo mwingine.
Basi achana na hilo la mkaa, chukua zako asali lita kuanzia 100 weka kwenye vibebeo safi na nembo yako pia, ingia Tabora au Singida uza ndani ya muda mfupi unarudi kufunga mzigo mwingine hiyo kumbuka ni chini ya wiki moja unaweza kuuza lita 100 za asali.
Chukua mafuta ya Alizeti kiasi cha kutosha ingia Mwanza piga biashara usisubiri serikalini ikuambie fursa, fursa ni nyingi sana hapo Dar ila wengi wamekariri fursa aina moja tu.
Kama kuna yeyote atakuwa tayari nitamsaidia alete biashara yake huku nitamsaidia kutafuta masoko. Pia mjaribu kwenye kilimo sio biashara tu.
Sent using Jamii Forums mobile app