Fursa za biashara zipo, vijana wa Dar es Salaam ni wazembe tu

Sasa hapo Wazembe ni Vijana wa Dar au Vijana wa Mikoani wanaokimbia yaliko mashamba na kwenda Dar kusiko na mashamba?!

Ukweli ni kwamba, Dar es salaam kuna vijana wengine baadhi ya mazao wanayajulia kwenye picha tu!!! Sasa nyie mnaozaliwa na kukua kwenye majembe lakini mkipata vi-bachelor degrees vyenu mnaanza kudharau majembe ndio hasa mlio wazembe!!
 
Yani utoe asali Dar ukauze Tabora au mi ndo sijaelewa hili viceversa?.
 
Tatizo ni moja tu linalotuumiza vijana wa dar.
Tunataka tufanye biashara zinazorudisha faida siku hiyo hiyo ili tuzipeleke kwenye anasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona kama unataka kutuingiza chaka, hivi asali ya kutoa wapi uipeleke Tabora au singida ukapige pesa? Au Mkaa wa kutoa wapi ukapige pesa Tanga? hv unadhani Tabora hakuna Asali? Au Tanga hakuna Mkaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…