DRC ni nchi ngumu sana kufanya biashara, wana kodi za kila aina, watu wengi (wageni) wanashindwa kufanya biashara huko, wenyeji wanafanya kwa sababu wanajuana kwa vilemba na wanajua jinsi gani ya kukwepa kodi
Naona kuna mdau anazungumzia vifaa vya electonics, hivyo vifaa pamoja na mambo ya nguo, viatu, perfum ni bidhaa za wenyeji kwa maana ndio biashara wanayoifanya kwa ufanisi sana huwa wanasafiri sana kwenda Dubai na Tanzania kuhemea hivyo vitu hasa nguo
Biashara ya vifaa vya ujenzi inalipa lakini pia inakufaa ujaribu kufanya visit huko ili upate soko,
Congo ni kubwa na haiko connected, kwa mfano watu wa Goma, Bukavu wanategemea sana cement, Nondo, na mabati kutoka Rwanda lakini hasa vitu vyao vinatoka Uganda, kwa bidhaa za chakula zinatoka hasa Kenya na Tanzania na Rwanda kidogo
Kwa upande wa Katanga province (Lubumbashi, Kolwezi, Likasi, Kalemie nk) nao wamegawanyika, baadhi ya Vifaa vinatoka Tanzania, lakini vingine ni Zambia na RSA kidogo
Kweli biashara hipo kubwa sema mazingira ya wageni kufanya biashara ni Magumu sana