Habari zenu wakuu
Ningependa kufahamu kwa wale wenye uelewa wa fursa za kibiashara zilizopo nchini uturuki karibuni tubadilishane mawazo, nategemea kwenda huko mapema mwezi wa tano kwa shughuli za kiofisi hivyo ningependa muda wa kupumzika nitumie kutafuta fursa za kibiashara huko.
Mengi nitajifunza nikifika huko lakini nikipata mawazo ya wazoefu hapa yatasaidia sana ili kufahamu pa kuanzia ni wapi. Baada ya kurudi itanipasa kuleta mrejesho ili kushare na watafutaji wenzangu
Karibu sana wakuu