Kaka hata unga wa sembe toka TZ ni mali huko Kenya kwani huko kuna dona tu,nina jamaa zangu ambao huniagizia niwatumia unga wamahindi huwa nawanunulia pale Manzese na hufurahia sana,pia pumba za mahindi ni biashara nzuri Kenya hasa kwa ajili ya chakula cha mifugo kwani kama nilivyosema hapo mwanzo wenzetu husaga unga wa dona kwa hiyo huwa hawana pumba,kuna Wakenya huja Manzese na hujaza malori hizo pumba.
Kama alivyosema mdau tatizo ni vibali huko mipakani,usumbufu ni mkubwa,hizo biashara huenda mjomba au shangazi wako awe waziri ndipo utafanikiwa