Fursa za kiuchumi Arusha mjini

The only

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
10,805
Reaction score
14,181
Mimi ni mfanyakazi,nimehamishiwa Arusha toka wiki iliyopita na kwa mfumo wa ofisi yangu ntahama baada ya miaka mitano ,naomba wadau mnijuze hivi naweza fanya biashara gani mtaji wangu ni mil 7 nilizolipwa kama transfer benefit,kila nachotaka kufanya nakuta kimesha fanywa tena kwa ubora ,biashara nayoifanya nikiwa mikoa mingine huwa ni baa ,lakini kwa hali ya uchumi ilivyo biashara naona si nzuri hapa Arusha ,ndo maana nikaona niwashilikishe mnidondoshee maujanja.
 
Ushauri: Arusha biashara karibu zote zimekamatwa na wazee wa kilimanjaro, kwa kifupi kubuni biashara Arusha mjini unatakiwa kukuna kichwa, labda ujaribu kuwa wakala mkubwa wa M pesa na uwe maeneo yaliyochangamka japo naona mtaji huo kama ni mdogo
 
Ushauri: Arusha biashara karibu zote zimekamatwa na wazee wa kilimanjaro, kwa kifupi kubuni biashara Arusha mjini unatakiwa kukuna kichwa, labda ujaribu kuwa wakala mkubwa wa M pesa na uwe maeneo yaliyochangamka japo naona mtaji huo kama ni mdogo
mwee umasikini umenikabili mimi
 
ongeza mil tatu iwe kumi nunua kirkuu mbili used za mil tano@, kirkuu kwa wiki inalaza laki, so kwa mwez utakua unalaza laki nane, pia kama we unapenda shughuli za kilimo lima horticulture products ambazo zinachukua miez miwil mitatu arusha zinakubali sana
 
Arusha na Moshi Mjini kama ni mgeni na unataka kufanya biashara uwe umejiandaa hasa kwa kubuni biashara ya maana na uwe na mtaji wa kutosha la sivyo utarukwa na akili ghafla.
 
Fursa za Arusha ni maandamano tu ya Lema .
 
Karibu arusha.
Tuliza akili kwanza.
Soma mazingira.
Changanya zakupewa.
Ungekuwa hujaajiriwa ningekupa idea ya mawe.
 
kilikuu ni bajaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…